Site icon A24TV News

WAANDISHI WA HABARI ZA KIMTANDAO WAPATIWA MAFUNZO YA KUANDIKA HABARI ZA SENSA KWA UMAKINI

Na Geofrey Stephen Iringa

Mhadhiri wa Shule Kuu ya Habari Chuo Kikuu Cha Dar es salaam (UDSM) Dk. Darius Mukiza amewapongeza waandishi wa habari za mitandao ya kijamii wanaoshiriki katika semina ya siku mbili ya Sensa ya watu na makazi inayofanyika kwenye Chuo Kikuu Kishiriki Cha Mkwawa mjini Iringa Kwa kazi kubwa iliyofanyika Jana katika kuripoti masuala ya sensa.

Amebainisha kuwa mmedhihirisha kwamba ninyi ni muhimu kwenye jamii katika kufikisha ujumbe husika na ndiyo maana Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imeanza kuwapa mafunzo nyie Kwa kuona umuhimu wenu.

“Jana Kila group la Whatsapp nililoingia au Facebook, Instagram,Blogs,YouTube na mitandao mingine ilikuwa na habari ya semina ya Sensa mjini Iringa mmeitangaza vizuri semina hiyo,” Amesema Dk.Mukiza.

Ameongeza kuwa ni matumaini yake kwamba kazi ya kuuhabairisha umma kuhusu sensa ya watu na makazi inatendelea mpaka tarehe 23, Agosti 2022 wakati ambapo kazi  ya sensa hiyo itakapofanyikika na ni wazi mtaendelea na kazi nzuri pia Kwa siku zijazo.

Mhadhiri wa Shule Kuu ya Habari Chuo Kikuu Cha Dar es salaam (UDSM) Dk. Darius Mukiza, Akizungumza na Waandishi mbalimbali wa mitandao ya kijamii wakati wa mafunzo maalum juu ya zoezi la Sensa yanayoendelea mkoani Iringa.