Site icon A24TV News

Mwenge wazindua Makao makuu ya Enduimet WMA na Kituo Cha kutoa taarifa kwa watalii.

Mwenge wazindua Makao makuu ya Enduimet WMA na Kituo Cha kutoa taarifa kwa watalii.

Mwandishi wetu, Longido

Mwenge wa Uhuru ,umezindua mradi wa majengo ya Makao Makuu ya Jumuiya hifadhi ya Wanyamapori ya Enduimet wilayani Longido ambao umegharimu kiasi cha sh 651.7 milioni.

Mradi huo ambao sasa utawezesha Enduimet WMA kuwa na Kituo cha taarifa za watalii umejengwa na Taasisi ya jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF) Kwa ufadhili wa shirika la uhifadhi la kimataifa(WWF-TCO).

Kiongozi wa mbio za mwenge Sahili Geraruma alipongeza TNRF na Enduimet WMA mwa kutelekeza mradi huo ambao unakwenda sambamba na jitihada za Serikali kukuza Utalii nchini.

Geraruma alitaka Enduimet WMA kutunza majengo hayo ili yatumike Kwa muda mrefu zaidi kusaidia sekta ya Utalii nchini.

Kiongozi huyo wa Mwenge alishukuru wafadhili WWF na wasimamizi na watekelezaji wa mradi Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF)Kazi nzuri ambayo wamefanya.

Akizungumza baada ya kuzinduliwa mradi huo, Mkurugenzi wa TNRF Zakaria Faustin alishukuru Serikali Kwa kutambua mchango na jitihada zao za kuendeleza uhifadhi nchini.

“Mradi huu ni sehemu tu ya miradi ya TNRF ambayo tunaifanya nchini katika maeneo mbalimbali ili kuendeleza uhifadhi Kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo”amesema.

Mwakilishi wa shirika la uhifadhi la WWF-TCO Professor Noah Sitat amesema wataendelea kufadhili miradi mingine Enduimet katika jitihada za kupunguza ujangili.

Mwisho