Author: arushatv

Na Geofrey  Stephen Simanjiro Mashahidi wawili katika kesi inayowakabili wafanyakazi sita wa mgodi wa madini ya Tanzanite wa Gem & Rock Venture unamilikiwa na Mfanyabiashara Maarufu Jijini Arusha,Joel Mollel maarufu kwa jina la Saitoti wameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilayani Simanjiro jinsi walivyopigwa na hatimaye kupoteza fahamu. Shahidi wa kwanza wa upande wa Jamhuri aliyejitambulisha kwa jina la Ezekiel Isack{30} mkaguzi wa migodi na baruti katika Wizara ya Madini alidai kuwa marchi 13 mwaka huu akiwa katika shughuli za ukaguzi katika mgodi wa saitoti ghafla alivamiwa na wafanyakazi wa Gem & Rock na kushambuliwa kwa vifaa vya uchimbaji na kujeruhiwa…

Read More

JAMII za pembezoni hapa nchini hasa za kifugaji zimetakiwa kutumia njia za asili wanazotumiaga kila siku kutatua migogoro mbalimbali katika jamii. Rai hiyo,ilitolewa jana jijini Arusha na Rose Njilo,Mratibu wa Shirika la MIMUTIE WOMEN ORGANIZATION(MWO),wakati wa maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Watu wa asili duniani ambayo yaliratibiwa na shirika hilo. Alisema kuanzia Januari mwaka huu wamefanikiwa kuwanusuru watoto 11 ambao walikuwa tayara kuozeshwa kwenye umri mdogo. Hata hivyo,alisema shirika hilo,limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa asilimia 75 kupambana na ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake hasa kupambana na ndoa za umri mdogo na mimba za utotoni. “Kama taasisi tumekuwa…

Read More

Na Richard Mrusha mbeya JESHI la kujenga Taifa (JKT) na wizara ya kilimo wametiliana saini mkataba wa mashirikiano katika kutekeleza mradi wa mashamba makubwa kuwezesha vijana kilimo biashara-Building a Better tomorrow (BBT) mbele ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na amiri jeshi mkuu Mh.Dkt. Samia Suluhu Hassan. Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa (JKT) Meja jenerali Rajab Mabele amesema jeshi hilo limeanza kutekeleza agizo la amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Dk.Samia Suluhu Hassan na kuhakikisha vijana wanaotoka makambini wanajengewa uzalendo wa kitaifa na kunufaika na fursa zilizopo katika…

Read More

Na Richard Mrusha mbeya MAMLAKA ya Huduma ya Usafiri wa Anga imewahakikishia watanzania kwamba usafiri wa sekta ya Anga ni usafiri salama zaidi kulikos ekta nyingine. Hayo yamesemwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushuari la watumiaji huduma za Usafiri wa Anga (TCAA-CCC) Innocent Kyara wakati akizungumza na waandishi wa habari siku ya kilele cha maoyesho ya wakulima katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya. “Sekta ya usafiri wa anga ndiyo sekta salama zaidi kushinda sekta nyingine za usafirishariji kutokana na nguvu kubwa iliyowekwa katika kuhakikisha bidhaa ,wananchi wanasafiri salama.”amesema Kyara na kuongeza kuwa “.Ajali za ndege hapa nchini zimekuwa…

Read More

Na Ahmed Mahmoud Kamishna wa Uhifadhi – TANAPA William Mwakilema amesema Maonesho ya Nanenane ni jukwaa sahihi la kutangaza vivutio vya utalii na fursa za uwekezaji vinavyopatikana katika Hifadhi za Taifa Tanzania kutokana na watu wengi wa ndani na nje wanaokuja kupata elimu na kununua bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wakulima, wafugaji na wafanyabiasha kutoka ndani na nje ya nchi. Ameyasema hayo katika banda la TANAPA leo tarehe 08.08.2023 alipoungana na watanzania wengine katika maadhimisho ya kilele cha maonesho ya wakulima almaarufu Nanenane yaliyofanyika kitaifa katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya. Akiwa katika banda la TANAPA na baadaye banda la…

Read More

Na Richard Mrusha mbeya Meneja Mauzo na Usambazaji kampuni ya mawasiliano TIGO Mkoa wa Mbeya, Ronald Richard amesema kuwa wanatumia fursa ya siku ya kilele cha maonesho ya kimataifa ya Nane nane 2023 katika Mkoa huo kuhamasisha wakulima kujiunga na TIGO ili kuwarahisishia shughuli za kilimo. Maonesho hayo yanafungwa rasmi leo Agost 8,2023 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na kauri mbiu ya mwaka huu ikiwa “Vijana na wanawake ni msingi imara wa mifumo endelevu na chakula”. Meneja mauzo na usambazaji Tigo mkoa wa mbeya Ronald Richard akizungumza na waandishi wa habari Aidha meneja…

Read More

Na Richard Mrusha mbeya AFISA mtendaji mkuu wa wakala wa Taifa hifadhi ya chakula NFRA Milton Lupa katika kuhakikisha kuwa usalama wa chakula nchini wana majukumu makubwa matatu ambayo kwanza ni kununua na kuhifadhi chakula na pili ni kutoa chakula wakati wa dharula ama wakati wa majanga yanayojitokeza ndani ya nchi na jukumu la tatu ni kuuza chakula ambacho muda wake wa kuhifadhi umekwisha ili kuweza kununua akiba mpya. amesema kuwa jukumu lingine walilopewa hivi karibuni na serikali ni kuhakikisha kuwa wanadhibiti mfumuko wa bei ambapo pale mahindi yanapokuwa bei ya juu wao wanatoa mahindi kwa bei ya chini ili…

Read More

Na Richard Mrusha mbeya KAMISHNA wa kinga na tiba Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini Dr. Peter Mfisi amesema kuwa wapo nane nane kwenye maonesho ya kilimo kwa sababu dawa za kulevya zipo za aina mbili kwamba kuna dawa za kulevya zinazotengenezwa viwandani kama heroin, kokein na dawa zingine lakini kuna dawa zingine zinatokana na kilimo kama bangi, Mirungi kwa hiyo ushiriki wao nane nane ni juu ya kuwaelezea wakulima kwamba wakati mwingine wasijihusishe na mazao hayo haramu kama bangi na mirungi. Amesema kuwa pia wapo kuwaonyesha jinsi bangi inavyoonekana na kubainisha kuwa kuna baadhi ya…

Read More