Site icon A24TV News

Vitambulisho vya machinga viaboreshwa vyaja kivingine

Na Mwandiwhi wa A24tv .

Wafanyabiashara wadogo mkoa Kilimanjaro wametakiwa kujitokeza muda utakapofika wa kujisajili na kupata vitambulisho ambavyo vitawasaidia mbalibali ikiwa ni kufanyabiashara bila ushumbufu wowote

Hayo yalisemwa na Wilesteven Kavishe katibu wa shirikisho la umoja wa machinga Tanzanian mkoa wa Kilimanjaro (SHIUMA) ,wakati wa mkutano wa Wafanyabiashara hao uliofanyika ujumbi wa Big Shark Bomang’ombe.

Katibu wa shirikisho hilo Wilesteven Kavishe Akizungumza na Wafanyabiashara hao

Akizungumza katika mkutano huo ambao umejadili mambo mbali mbali ya maendeleao ikiwamo uchaguzi wa Serikali za mitaa na ujio wa Mwenge wa uhuru,amewataka Wafanyabiashara muda utakapofika wajisajili na kupata vitambulisho hivyo

“Ni kweli tunategemea mwezi March mwaka huu utaratibu wa usajili unaweza kuanza hivyo ni muhimu kujitokeza , Wafanyabiashara watapewa semina kila Wilaya na Maeneo yao kabla ya kuanza zoezi hilo”amesema Kavishe

Kavishe amesema vitambulisho hivyo vinatolewa na Serikali ,kwa sasa vimeboreshwa badala ya kulipa kwa mwaka mmoja kwa sh,20,000 Sasa unakaa nacho kwa miaka mitatu,na kwamba vitambulisho hivyo kimeongezewa ubora na ufanisi,kinatambulika maeneo mengi ikiwamo sehemu ya Afya na bank.

“Ni kweli vimeboreshwa badala ya kulipa sh,20,000 kwa mwaka mmoja kwa sasa unalipa sh,20,000 unakaa nacho kwa muda wa miaka mitatu ,tunamshukuru Rais Samia Suluhuu Hassani kwa kutujali Wafanyabiashara wadogo amesema Kavishe

Nawaomba muda utakapofika wajitokeze na kama mtu hatajitoze,inamaana baadaye kutakuwa na ukaguzi ,na ukaguzi huu utabaini wale ambao hawana vitambulisho ina maana wapo kinyume na utaratibu wa Nchi yetu

Mwenyekiti wa shirikisho hilo Wilaya hapa,Paul Malongo,amesema mbali na vitambulisho hivyo amewata Wafanyabiashara hao kujitokeza kushiriki mbio za Mwenge utakapofika Wilayani humo ,ambapo pia watazindua bidhaa zao.

“Ni kweli tutakuwa na mabada ya biashara kwenye eneo la mkesha wa Mwenge tumewataka Wafanyabiashara wajisajili mapema ,waone viongozi wao watapewa muongozo iliwa ni pamoja na malipo “amesema Malongo.

Pia amewataka kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa wenye kauli mbio ,tunza mazingira na shiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa ujenzi wa Taifa endelevu

Mwisho