Site icon A24TV News

RAIS DK.MWINYI AWASHUKURU JUMUIYA YA ZAWIYATU QADIRIA

Na Mosses Mashala Zanzibar .

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi amewashukuru Jumuiya ya Zawiyatu Qadiria Tanzania kwa kumuombea Dua Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika ibada ya Sala ya Ijumaa Msikiti wa Masjid Ngamia Welezo Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe: 15 Machi 2024.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amehimiza umuhimu wa kuendelea kuiombea Dua Nchi na kudumisha amani na utulivu.