Site icon A24TV News

MATUKIO KATIKA PICHA SOMALIA ILIVYO JIUNGA RASMI MWANACHA WA EAC WAPATA MAPOKEZI MAKUBWA

Na GEOFREY STEPHEN ARUSHA
Nchi ya Somalia imejiunga Rasmi kuwa mwanachama wa nane wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika makao Makuu ya EAC Jijini Arusha na kuelezwa kuwa itasaidia suala Zima la msukumo wa changamoto za ajira kwa Nchi wanachama pamoja na kupanua soko la pamoja .
Aidha Kujiunga kwa Somalia ni kutokana na kikao cha Wakuu wa nchi kilichoketi  November 24 mwaka Jana jijini Arusha,kukubali Nchi hiyo kujiunga na jumuiya ya Afrika Mashariki.
Akiongea na waandishi wa habari Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Dkt.Peter Mathuki katika sherehe fupi ya kupandisha bendera na kupokea hati za unachama wa Somalia makao makuu ya EAC Jijini Arusha amesema soka la Jumuiya limepanua wigo na kuwa na watu takribani milioni 350 kwa Sasa na hivyo kuiwezesha jumuiya hiyo kujipanua kibiashara.
Aidha alisema kiwango cha ukuaji wa pato la EAC limeongezeka kutoka Dolla bilioni 2.5 Hadi Dola bilioni 3 na kuongeza soko la ajira kuondoa changamoto za ukosefu wa ajira kwa nchi wanachama na ongezeko la bidhaa kwa kuwa na watu milioni 350 kwa sasa.
Akiongelea suala la usalama Dkt.Mathuki amesema kuwa kuongezeka kwa soka hilo la watu wanaofikia milioni 350 kutaondoa changamoto za upungufu wa ajira na kupelekea wananchi kuchangamkia uzalishaji wa bidhaa na kuuza katika soko la pamoja.
“Hii ni Moja ya kuondoa changamoto za ajira na kurudisha Hali ya usalama katika mataifa ya Jumuiya ikiwa soko la Jumuiya kwa Sasa Lina watu takribani milioni 350 uzalishaji wa bidhaa utaondoa upungufu na kuzalisha ajira hivyo kuwepo kwa usalama katika nchi zetu”
Kwa Upande wake Waziri wa Habari wa Somalia Daud Aweso amesema wanayofuraha Kubwa kukamilisha safari ndef⁰mu ya miaka 12 na safari hiyo ilikuwa na Kazi Kubwa ya changamoto lakini hawakuchoka kufikia hatua hiyo ya kukamilisha utaratibu wa mwisho wa kujiunga na EAC.

Alisema Jumuiya hiyo itakuwa na manufaa makubwa kwa Somalia na nchi zote wanachama kwa kuwa nchi ya nane kujiunga na Jumuiya hii na tunaleta mchango Mkubwa tutakaotoa kuleta maendeleo ndani ya nchi zetu katika uchumi biashara n.k.Ameeleza kwamba changamoto zipo ndani ya Somalia tunaendelea kuzifanyiakazi na Kwa mwaka uliopita Kuna mambo mengi tulioyafanya kuhakikisha tunawapa Picha nzuri wanachama wengine kukiwa na wanachama zaidi ya 350.

Awali Waziri wa viwanda na biashara wa Somalia,Jibril Abdirashid Haji Abdi amesema wanaendelea na wanayofuraha kuwa sehemu ya nchi nane za Jumuiya hiyo ya EAC na wanashukuru kwa kukaribishwa Rasmi na kuahidi kushirikiana na nchi zengine za Jumuiya hiyo kukuza uchumi.

Mwisho