Site icon A24TV News

DIWANI WA MJINI KATI TOJO ATOA MSAADA HOSPITAL KATA YA DARAJA MBILI KWA KUGAWA MASHUKA YA KUJIFUNIKIA WAGONJWA

Na Geofrey Stephen Arusha .
Diwani wa Kata ya Mjini Kati jijini  Arusha, Abdu Tojo amejitolea msaada wa Mashuka 60 kwa ajili ya kukisaidia kituo cha Afya cha daraja mbili,baada ya kubaini uwepo wa uhitaji  na kuwaomba wadau wengine wa Afya kujitokeza kusaidia maeneo yenye uhitaji.

 

 
Tojo ambaye amekuwa mdau mkubwa wa kusaidia sekta ya afya,mwishoni mwa mwaka jana alisaidia mashuka na blanketi katika kituo cha Afya Kaloleni baada ya kupokea uhitaji , ambayo yalisaidia akina mama wanaojifungua kuwasitiri na baridi kali.


Akiongea mara baada ya kukabidhi msaada huo,kwa mganga mfawidhi wa kituo hicho, Luciana Kazimoto, Tojo alisema msaada huo hauna lengo la kujijenga kisiasa bali ni moyo binafsi wa kujitolea kwa kushirikiana na wadau wa afya unaomsukuma kusaidia jamii yenye uhitaji.
 

“Nimetoa msaada huu sio kwamba nahitaji sifa  za kisiasa ila  nimeguswa na uhitaji wa kituo hiki cha afya na sihitaji kujijenga kisiasa bali nitalipwa na mwenyezi mungu na niwaombe wengine  wajijengee utamaduni huu na mungu atawalipa”

 
Akipokea msaada huo mganga Mfawidhi wa kituo hicho cha afya Daraja mbili, dkt Lusiana Kazimoto alimshukuru diwani huyo kwa msaada alioutoa kwani kabla ya mashuka hayo changamoto ilikuwa ni kubwa ila wanaimani msaada huo utapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto hiyo.


Kwa niaba ya watumishi wa afya namshukuru sana diwani Tojo kwa moyo wake wa ukarimu ambao umekuwa chachu ya maendeleo”
 
Alizitaja changamoto zinachokikabioi kituo hicho cha Afya ni pamoja na upungufu wa wodi za kulaza wagonjwà akidai kwamba eneo hilo linakabiliwa na uhalifu mwingi ambao umekuwa ukisababishwa na vibaka kujeruhi watu kwa visu na mapanga .
 
Naye diwani wa kata hiyo ya daraja mbili, Prosper Msofe alisema changamoto hizo zimeanza kufanyiwa kazi ikiwemo ujenzi wa jengo la juu litakalosaidia kupata nafasi kubwa ya kulaza wagonjwa ukizingatia ufinyu wa eneo la kituo hicho. 


Mwisho