Site icon A24TV News

Baraza kuu la WaislamuTanzania ( BAKWATA), mkoa wa Kilimanjaro kuanza kutoa elimu ya ndoa

Na Wandishi wa A24Tv.

Moshi,Baraza kuu la WaislamuTanzania (BAKWATA), mkoa wa Kilimanjaro limesema litafanya semina ya elimu ya Ndoa kwa viongozi kuanzi ngazi ya Msikiti,Kata na Wilaya baada ya kugundua kwamba jambo elimu ya Ndoa imekuwa ndogo nakusababisha migogoro kuongezeka na familia kusambaratika

Haya yamesemwa na Hussein Chifupa Kadhi wa mkoa huu wakati wa uzinduzi wa jengo la Ofisi ya BAKWATA Moshi mjini Mara baada ya kufanyiwa ukarabati ,na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwamo wa Dini.

Akizungumza Mara baada ya uzinduzi huo,amesema watafanya ziara Wilaya zote mkoani hapo kwa lengo la kutoa elimu ya hiyo kutokana na baadhi ya Ndoa kusambaratika na kusabisha watoto kuteseka na wengine kukimbilia mitaani

“Ni kweli tunatatua maswala mbali mbali ikiwamo swala la wanandoa katika uchunguzi tunaketi ndani ya vikao vyetu jambo kubwa linalochangia ni elimu ya ndoa imekuwa ndogo, baada ya kuona tunaanza ziara kufanya semina kwa lengo la kutoa elimu ya hiyo “amesema Chifupa

Chifupa amesema tunafahamu ndoa ni taasisi muhimu sana inayotengenza jamii inayotengenza kizazi inayotengenza Taifa ,Taifa linakuwa nzuri maana yake taasisi ya ndoa inatakiwa kuwa imara,tunakwenda kuwajengea uwezo vingozi kuhusu ekimu hii ili na wao waweze kuwafikishia waumini.

Amesema ndoa ikivunjika unasababisha mambo mengi watoto wanakosa malezi ya wazazi wawili wengine wanakimbilia mitaani na kuanza kujifunza mambo maovu lengo la Baraza ni kurudisha amani kwa wale ambao kidogo amani imepotea juu yao

Sisi kama Baraza tunatoa maelekezo kwa maimamu wa misikiti,mashekh wa Kata na Wilaya na wale wote wenye mamlaka ya kuweza kusimamia kufungisha ndoa wajiandae kwa semina hiyo pindi watakapofika katika maeneo yao ili kunusuru ndoa na kubaki salama

Issa Juma Katibu wa Kadhi ,amesema kwa kiindi kuanzia January hadi March mwaka huu ,wamepokea malalamiko ya ndoa 12 na yote wamewaza kusuluhisha na baadhi ya wanandoa wamerudi na kuishi pamoja

Amesema semana wanayokwenda kuifanya ni kuimarisha vikao vya chini kwa ajili ya hizi suluhuu kwa sababu imekuwa ndoa haziishi zinakuwa ni za muda mfupi kwa hiyo ziara yetu kikubwa ni kwenda kuimarisha vikao vya chini ili kusimamia ndoa ,malezi

Awazi lema katibu wa BAKWATA mkoani hapo ,amese jengo hilo lilijengwa mwaka 1975,lilichakaa na kuhitaji ukarabati,aidha amewataka viongozi wa BAKWATA ngazi mbali mbali kusimamia kwa makini mali za chama zilizopo kwenye maeneo yao.


Mwisho.