Site icon A24TV News

RAIS DK.MWINYI ASHIRIKI DHIFA YA RAIS WA POLAND

Na Mwandishi wa A24tv .

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ameshiriki dhifa ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa heshima ya mgeni wake Rais wa Poland Mhe.Andrzej Sebastian Duda. Ikulu Dar es Salaam tarehe :09 Februari 2024.

 

Katika hafla hiyo Rais Dk.Mwinyi amesalimiana na viongozi mbalimbali wa Serikali, Vyama vya siasa, Dini na Wastaafu.

Aidha baada ya kushiriki hafla hiyo Rais Dk.Mwinyi anatarajiwa kurejea Zanzibar.

Mwisho