Site icon A24TV News

RAIS SAMIA ALIVYO ONGOZA MAZISHI YA HAYATI LOWASA NGARASHI ARUSHA RAIS MWINYI AMLILIA

Karibu kutazama matukio katika picha viongozi wakiongozwa na Mh Rais Samia Suluhu Hassan katika Mazishi ya Hayati Edward Lowasa kijijini Ngarashi Wilayani Monduli Mkoani Arusha .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua kwenye kaburi la Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowassa katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa Marehemu Monduli Mkoani Arusha tarehe 17 Februari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka udongo kwenye kaburi la Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowassa Monduli Mkoani Arusha tarehe 17 Februari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi wengine katika mazishi ya Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowassa, Monduli Mkoani Arusha tarehe 17 Februari, 2024.


Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye mazishi ya Hayati Edward Ngoyai Lowassa yaliyofanyika nyumbani kwa Marehemu Monduli Mkoani Arusha tarehe 17 Februari, 2024






Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ameshiriki maziko ya Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowassa nyumbani kwake Kijiji cha Ngarash Wilaya ya Monduli, Mkoa wa Arusha tarehe 17 Februari 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan ameongoza waombelezaji katika maziko hayo.

Viongozi mbalimbali wa Serikali, Wastaafu, Dini, Kimila, Vyama vya siasa, Vyombo vya ulinzi na usalama wameshiriki maziko hayo.

Majane wa Marehemu, Mama Regina Lowassa, akiwek shada la maua kwenye kaburi pa mume wake mpendwa Hayati Edward Lowassa, wakati wa Ibada ya mazishi, iliyofanyika nyumbani kwake Kijiji cha Ngarash wilaya ya Longido leo Februari, 17, 2024.

Mawaziri wameungana na waombolezaji wakiwa kwenye ibada maalum ya mazishi ya Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowassa, nyumbani kwake kijiji cha Ngarash wilaya ya Monduli.

Ibada hiyo ya mazishi inaongozwa na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kulutheri Tanzania, Askofu Dkt. Alex Geras Malasusa.

Hayati Edward Ngoyai Lowassa, amefariki dunia Februari 10, 2024, katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ya Jijini Dar es salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu.

MWisho .