Site icon A24TV News

SERIKALI KUBORESHA MAKTABA 22 NCHINI

Na Mwandishi wa A24tv.

Serikali imetenga takriban Shilingi Bilioni 2 kwa kuboresha Maktaba 22 ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa kuboresha Maktaba zote nchini ili kutoa fursa kwa wanafunzi, walimu na wakazi wengine wa ndani na wanaoishi nje ya nchi kupata maarifa.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda akizindua Maktaba iliyojengwa na …… ugweno……kwa ajili ya wanafunzi na wananchi wa Eneo hilo.

Akizungumza katika hafla hiyo Prof. Mkenda amesisitiza kuwa wadau Binafsi wanakaribishwa kuwekeza katika kujenga Maktaba maeneo mbalimbali Nchini na kuwashukuri wadau waliojitoa kushiriki kujenga Maktaba hiyo ya Ugweno.

Maktaba hiyo iliyogharimu ….. imejengwa na

“Maktaba hii inayoitwa Martha Onesmo, ni kwa ajili ya kumuenzi bibi yangu, ni ndoto niliyoota tangu nasoma kidato cha sita, ninafuraha kuwa ndoto hiyo imetimia. Maktaba hii pia ni mchango wangu na wale walioniunga mkono, katika kuunga mkono juhudi za serikali zinazolenga kuboresha sekta ya elimu nchini”.alisisitiza.

Maktaba imesimama kwa michango kutoka kwa wanajumuiya wa Msangeni itakuwa kituo cha mafunzo ya ujasiriamali na elimu ya aina nyingine kwa ujumla itakayochangia maendeleo ya taifa na kutoa wito kwa Watanzania wote kujenga tabia ya kutumia huduma za maktaba kujisomea ili waweze kupata maarifa na kuachana na dhana potofu kuwa maktaba ni za wanafunzi, walimu na wasomi pekee.

Alitoa shukrani kwa wafadhili mbalimbali waliomwezesha kutimiza ndoto yake baadhi yake akiwataja kuwa ni pamoja na Bayport Tanzania, Barick Gold Tanzania, Dayosisi ya Mwanga ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT-MD).
Akizungumza katika hafla hiyo Askofu wa KKKT wa Dayosisi ya Mwanga Askofu Chediel Sendoro, alimpongeza Bi Jennifer, kwa ubunifu wake ambao alisema utachangia maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

“Maktaba hii ijapokuwa ipo kwenye jengo la Kanisa itatumika kwa watu wote bila kujali imani zao za kidini, lengo ni kuhakikisha kila mtu anapata fursa ya kujiendeleza na kupata maarifa ya ziada kwa ajili ya maendeleo yake binafsi na taifa kwa ujumla,” alisema.

Aidha aliwapongeza wazazi wa Bi Jennifer Dickson na Dk. Linda Ezekiel, kwa malezi mazuri ya wazazi waliyompa binti yao ambayo yalimwezesha yeye (Jennifer) kuja na maono yenye lengo la kuchangia maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

“Nichukue fursa hii kuwataka wazazi wengine kuiga mfano wa wazazi wa Jennifer; pia niwasihi watoto wengine kuiga mfano wa Jennifer ili taifa liendelee kupiga hatua kupitia vijana wetu”, alisema.

 

Kwa upande wake Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof Bonaventure Rutinwa, amesema kuwa maktaba hiyo ni miundombinu ya kielimu inayomwezesha mtu wakiwemo watoto wadogo kupata elimu ya ziada kupitia usomaji wa vitabu, ambapo alisema ni vyema watoto wakaanza kusoma. kufahamishwa kuhusu umuhimu wa kutumia maktaba mapema katika hatua za utotoni.

“Tunasoma sio kupata elimu ya shule pekee bali kuboresha maisha yetu kwa ujumla na hii ni moja ya maana halisi ya kuwepo kwa maktaba kuwa;maktaba zimekusudiwa kwa ajili ya watu wote na si kwa ajili ya wanafunzi na walimu pekee”,alisisitiza.

Mwisho.