Site icon A24TV News

WAZIRI WA JUMUIYA AFRIKA MASHARIKI HALA KIAPO CHA KUTUMIKIA JUMUHIYA NITAKUNGANISHA USHIRIKIANO NCHI ZETU

Na Geofrey Stehen Arusha .

Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka (Kenya) Peninah Malonza ameshukuru baada ya kula kiapo cha kutumikia Bunge la Afrika Mashariki EALA na kuahidi kuchapa Kazi kwa weledi na maarifa sanjari na kutoa ushirikiano kuipeleka mbele Jumuiya hiyo.

Aidha amejibu hoja ya Mawaziri kuwa Watoro iliyotolewa kwa kusema mawaziri wengi wanayo majukumu mengi ndani ya serikali zao hivyo wanakazi zaidi ya Moja tena Kubwa hivyo tutashauriana na kupeana moyo wa kufika katika vikao maana tutaweza kusukima maendeleo.

Ameyasema hayo mara baada ya kuapishwa katika Bunge la Afrika Mashariki EALA Jijini Arusha katika Mkutano 1 kikao cha pili cha Bunge la 5 la EALA

Ameahidi kutoa ushirikiano kwani Taifa la kenya lipo mstari wa mbele kutengeneza Jumuiya yetu iende mbele kwa kushirikiana na Mataifa yanayunda Jumuiya hiyo.

“Naihidi kutoa ushirikiano kwa nafasi hii niliyopewa au majukumu ntakayopewa katika Baraza la mawaziri wa Jumuiya yetu kupeleka gurudumu la Mtangamono wa Afrika Mashariki”

kwa Upande wake Mbunge  kennedy Musyoka  Kalonzo amesema wamepokea kwa furaha kubwa sana kiapo cha waziri penina na wanategemea kuona mchango mkubwa kutoka kwake wa kuunganisha jumuhiya ya africa mashariki

amesema kwamba wamejifunza mengi kupitia Bunge la EALA baada ya kushuhudia kuapishwa kwa Waziri wao bungeni humo sanjari na bajeti ndogo ya nyongeza.

Amesema kwamba kwa kipindi cha siku mbili walizokuwapo bungeni hapo kujifunza nakusema Umoja uonekane ambapo ameziomba nchi Wanachama kulipa kipaumbele suala la wafanyakazi wa Jumuiya hiyo kutofanya Kazi kwa mkataba na badala yake kuajiriwa.

” Ukiangalia wafanyakazi wa Bunge na wale wa Mahakama wanafanyakazi kwa Mkataba pengine wanalipwa fedha mingi huku wengine wakitumika kwa miaka 5 hadi kumi lakini ukiondoka inakuwa ngumu kupata ajira nyingine tungelipenda watumishi hao kuanza kuajiriwa na kupata mafao pindi wakimaliza ajira zao na kuondoa suala hilo la mkataba”

Amesisitiza suala Zima la kuboresha soko la pamoja ikiwemo kutumia ukubwa uliyokuwa nalo la idadi ya wakazi wa Jumuiya hiyo takribani watu milioni 300 kupeleka bidhaa zinazozalishwa ndani ya Mataifa 7 kuboresha sarafu ya pamoja badala ya kutumia Dola kubadilisha fedha tununue kwa fedha zetu za Mataifa yetu ili kutotumia fedha hiyo Dola

Mwisho .