Site icon A24TV News

NAIBU KATIBU MKUU OFISI YA RAISI DKT MAHERA AWATAKA WAKUU WA VITUO VYA AFYA NCHINI KUFUNDISHA KWA NIDHAMU , ZINGATIENI MAADILI.

Na Geofrey Stephen.Arusha 
Naibu katibu Mkuu ofisi ya Rais Tamiseni anayeshughulikia Afya dkt  Charles Mahera amewataka wakuu wa vyuo vya Afya hapa nchini kuongeza jitihada za kufundisha nidhamu ,wadilifu na hofu ya mungu kwa wahudumu wa afya (Nesi)ambao alidai  wanaongoza kuwa na Lugha mbaya kwa wagonjwa na kusababisha vifo.

Dkt Mahera ameyasema hayo jijini Arusha wakati akifungua mafunzo ya wiki mbili kwa wakuu wa vyuo vya afya vya serikali kutoka mikoa mbalimbali nchini yanayofanyika katika chuo cha Afya cha CEDHA.

Naibu waziri alisitiza kuwa ni wajibu wa watoa huduma za afya kuwa na weledi utakaoendana na kasi ya uboreshaji wa huduma za afya ili kwendana na uwekezaji mkubwa unaofanywa na rais Samia Suluhu katika sekta hiyo,hivyo wakuu wa vyuo hivyo  .

Aliwataka wakuu wa vyuo kufundisha wahuduma wa Afya namna ya kujali wagonjwa, akili hisia na uwajibikaji.

Katika hatua Nyingine dkt Mahera alisema serikali imejikita kuwekeza katika sekta ya Afya kwa kuweka vifaa tiba, ujenzi wa za zahanati takribani 6000,ujenzi wa vituo vya afya kutoka 400 hadi 755 na wamejipanga kujenga vituo vingine vya afya vipatavyo  214 mwaka ujao 2024.

Aidha alisema  serikali imefanikiwa pia kujenga hospitali za wilaya kutoka 77 hadi 177.

Awali mkuu wa Chuo hicho cha Afya cha CEDHA Dkt Johannes ,Lukumay,alisema kuwa  mafunzo hayo yamekuwa na mwitikio mdogo Kutoka Katika timu za usimamizi  na uendeshaji  wa huduma za afya kuanzia ngazi ya taifa hadi halmashauri Vituo vya kutokea huduma za afya  na Vyuo vya afya Nchini.

Hivyo akaiomba Serikali kupitia Kwa Naibu Katibu mkuu Tamisemi,kuziwezesha  na kuzielekeza  taasisi na sehemu za kutokea huduma zilizoko chini ya  ofisi yake kutenga  fedha za kuwezesha timu  za usimamizi. na  uendeshaji  wa huduma za afya  ziweze kupata mafunzo  hayo yanayotolea na Chuo hicho.

Alisema kuwa mafunzo hayo yanawalenga Viongozi wa Sekta ya afya ngazi mbalimbali  kuanzia makao makuu ya Wizara ya afya ofisi ya Rais,Tawala za mikoa na Serikali za mitaa,Wakuu wa Vyuo  vya afya na wasaidizi wao,waganga Wakuu wa mikoa ,hospitali za rufaa za mikoa pamoja na timu za uendeshaji  wa huduma za afya ,waganga Wakuu wa Wilaya na waganga wafawidhi wa Wilaya pamoja na timu zao za uendeshaji  huduma za afya  na Vituo vya kutolea  huduma za afya.

Alisoma Ili kuimarisha utawala bora,Uongozi na manejimenti ya usimamizi wa  huduma za afya  Kwa kushirikisha Kamati za Ulinzi  na Usalama  na Viongozi  na watendaji wa Serikali  katika ngazi za Viongozi Wakuu wa halmashauri,wakiwemo Wenyeviti na Wakurugenzi  wapatiwe mafunzo ya manejimenti,Uongozi na utawala Ili kuwepo  uelewa endelevu wa pamoja katika kusimamia  na kuendesha  huduma  bora za afya kwa ngazi ya msingi.

Mwisho .