Site icon A24TV News

LUSHOTO KUJENGWA MAHAKAMA YA KISASA.* *NI KUFUATIA WAZO LA DC KALIST LAZARO KWA JAJI MKUU WA TANZANIA

Na Mwandishi wa A24tv Lushoto
Novemba 24, 2023.

Mahakama ya Kisasa Wilayani Lushoto itakayotumika kwa shughuli za Kimahakama pamoja na kuwa sehemu ya utoaji Mafunzo kwa wanafunzi watakaopita katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) kilichopo Wilayani Lushoto inatarajiwa kujengwa muda wowote kuanzia sasa.

Kauli hiyo imetolewa na Mgeni Rasmi Jaji Mkuu wa Tanzania *Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma* alipokuwa alihutubia katika Mahafali ya 23 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama (Institute of Judicial Administration) – IJA yaliyofanyika leo tarehe 24/11/2023 chuoni hapo. Wanafunzi wapatao 800 wa ngazi mbalimbali ikiwemo Shahada wamehitimu leo.

Mhe. Jaji Mkuu emeeleza kufurahishwa na wazo alilotoa Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mhe. Kalist Lazaro jana ambapo ameshauri kujengwa mahakama hiyo ya kisasa, na tayari eneo la kujenga limeshapatikana.

Profesa Ibrahim anasema _”… Dr. Kalist Lazaro ni mwana IJA namba moja. Jana wakati wa kunipokea alijenga hoja kwa niababa ya chuo chetu (IJA) akisema, Polisi tayari wana jengo jipya la kuvutia, pengine kuliko majengo yote mapya yanayojengwa ya Polisi nchini Tanzania. Na akasema, Mahakama ya Lushoto ipatiwe jengo jipya. Jengo hilo liwe sehemu ya kuwapatia mafunzo wanafunzi wanaopita IJA…”_. Amesema Profesa Ibrahim Juma akinukuu Maneno ya DC Kalist Lazaro.

Mhe. Jaji Mkuu anaongeza kusema, *_”Kwa kawaida hii lugha tulitegemea itoke kwa mwana-IJA mwanafunzi, mhadhiri au baraza la chuo. Lakini Mhe. DC ameona umuhimu wa Elimu inayotolewa hapa kwa Jamii, na vilevile umuhimu wa kuwa na Mahakama ya kisasa itakayokuwa ya Mafunzo”._*

_”Lakini ameenda mbali zaidi (DC Kalist Lazaro) kwani kuna kikundi cha wananchi kijulikanacho kama *Lushoto Coffee Growers Association* wametetoa eneo lenye mita za mraba 8,499 kwa ajili ya kujengwa mahakama hiyo”._

Kwa upande mwingine, Mgeni Rasmi – Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma katika Mahafali hiyo amesema, “Siku za Mahafali ni wakati mzuri wa kujitathimini”.

“IJA kinapotekeleza malengo yake kwa ubora , Mahakama ya Tanzania hujizolea sifa”.

” Na chuo chetu kila mara ninapohudhuria mikutano pamoja na viongozi wa Mahakama za nje, huwa wanapenda kutafuta muda kutembelea chuo hiki cha Lushoto.” Amesema Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma.

#Miundombinu Bora ya Mahakama,
#Mazingira Bora ya utiaji wahaki

Mwisho