Site icon A24TV News

KIRUNGU CHASABABISHA TAHARUKI BARAZA LA MADIWANI MOSHI

Na Mwandishi wa A24tv .

Moshi.Baraza la Madiwani Manispaa ya Moshi limepata taharuki baada ya aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Moshi na Diwani wa Kata ya Bomambuzi Mh Juma Raibu kuingia na fimbo iliyodhaniwa ni ile ilikuwa ikitumika na Mwalimu Nyerere jambo ambalo liliamisha mjadala uliokuwa unajadiliwa na kuijadili fimbo hiyo huku imani za kishirikina zikitajwa huku wengine wakishindwa kutoa taarifa kwa usahihi na kuaingizia fimbo hiyo

Akizungumza nje ya kikao cha baraza Katibu wa Baraza la madiwani Witness Mzirai alisema fimbo hiyo iliibua taharuki huku akisema kuwa fimbo hiyo haina shida yoyote kama baadhi ya watu walivyoihusisha na imani za kishirikina bali ni fimbo ambayo inatenda haki, uhalisia,upendo na amani imani kama ambavyo ilikuwa ikitumia na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Bomambuzi Juna raibu alisema fimbo hiyo amepewa na wazee maalumu kutoka kabila la Wazanaki kwa ajili ya kusimamia haki,ueledi utii ubunifu,pamoja na kutetea maslahi ya serikali na umna ili kutafsiri matamanio ya hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na haina imani za Kishirikina kama baadhi ya madiwani walivyoamini.

Mwisho