Site icon A24TV News

KATIBU WA CCM MKOA WA ARUSHA AWAONYA WAGOMBEA NAFASI YA MWENYEKITI MKOA ! KUPAKANA MATOPE ,MUDA WA KAMPENI BADO

Na Geofrey Stephen Arusha 

Zoezi la kuchukua Fomu limefungwa Rasmi jana November 23 Majira ya Saa kumi kamili za jioni huku  Makada wapatao 83 wa chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Arusha wakirejesha Fomu za kuwania nafasi ya mwenyekiti wa ccm mkoani  wa Arusha iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mwenyekiti Marehemu ZELOTHE STEPHEN  ZELOTHE. 

Akiongea na vyombo vya habari baada ya zoezi hilo la kurejesha fomu kukamilika katibu wa ccm Mkoa ,Mussa Matoroka alisema kuwa jumla ya wanachama 88 walijitokeza kuchukua fomu lakini waliofanikiwa kurejesha ni 83.
Alisema mwitikio ulikuwa mzuri ikiwa ni haki ya msingi ya kila mwanachama wa chama chamapinduzi Ccm  mwenye sifa kugombea kwa ajili ya kukitumikia chama hicho.
 
Matoroka amesema kwamba taratibu zingine za kuchuja wagombea kulingana na sifa zao zitafanyika na mchakato wa kumpata mwenyekiti itatangazwa hatua kwa hatua.
Aliwasihi wagombea wote wanaowania nafasi hiyo kutojihusisha na siasa za kupakana matope ikiwemo kucheza rafu na kutoa rushwa kwani kwa kufanya hivyo ni kuhatarisha nafasi waliomba .
Nafassi ya kuchukua fomu ilianza juzi Novemba 21 hadi 23 ikiwa ni wiki tatu na siku kadhaa tangu kufariki kwa aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo ZELOTHE STEVEN aliyefariki kwa maradhi Oktoba 26 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Mwisho .