Site icon A24TV News

RAIS SAMIA KUFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAJAJI WA NCHI ZA KUSINI MWA MASHARIKI YA AFRIKA JININI ARUSHA

Na Geofrey Stephen Arusha

KIKAO kazi cha Watendaji Wakuu wa Mahakama kutoka   Nchi za Kusini Mwa  Mashariki ya  Afrika (SEAJAA) kitafanyika Oktoba 22, 2023 Jijini Arusha

Kikao kazi hicho kitakua na mada mbali mbali ambazo zitawasilishwa ni pamoja  na ajenda za marekebisho ya katiba ya chama hicho ikiwemo uboreshaji wa vyanzo vya fedha, uboreshaji wa mtandao wa chama hicho,

Madazingine ambazo zitajadiliwa katika kikao kazi hicho ni pamoja na maswala ya fedha huku nchi 13 za umoja huo zitakazoshiriki mkutano huo ni pamoja  Angola, Botswana, Lesotho, Zanzibar, Shelisheli, Zimbabwe, Malawi, Msumbiji, Eswatini, Zambia, Namibia na mwenyeji Tanzania.

Akiongea na mapema leo hii na vyombo vya habari Mh Mwenyekiti wa Chama cha Watendaji Wakuu wa Mahakama wa Nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEAJAA) Profesa Elisante ole Gabriel ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, amesema maandalizi ya kikao cha watendaji hao yanaendelea kabla ya Mkutano utakaofunguliwa Oktoba 23 na Rais Samia Hassan Suluhu.

 

Alisema ushirikiano huo kati ya maofisa hao ndio unaosababisha ufanisi zaidi katika utoaji wa haki na utendaji kimahakama

Profesa Gabriel amesema kikao cha 13 zimejiunga na chama hicho huku jitihada za nchi nyingine tatu kujiunga na chama hicho zikiendelea na badae idadi ya wanachama wengine itaongezeka kufika Afrika nzima

Amesema kikao kazi hicho kitajadili mambo mbalimbali kwani watendaji wakuu wanawashauri majaji wakuu katika masuala ya miundombinu, rasilimali za watu na masuala ya fedha

Mwisho