Site icon A24TV News

NI HISTORIA MSANII MAMA NAIRO ALAMBA DILI NONO NA CASSANDRA, LINGERIE MWANAMKE MVUTO NDANI YA NYUMBA !

Na Geofrey Stephen Arusha.

Ni Mama Nairo Alisimamisha Jiji la Arusha baada ya kusaini mkataba mnono  na duka la kisasa la kuuza nguo za kike la Cassandra Lingerie la jijini Arusha

Mama Nairo wakati wa kusaini dili hilo aliingia  katika viunga vya Hotel ya kitalii ya SG Resort kwa madaha huku akiwa na ulinzi mzito ambao uliwashangaza watu waliofika kushughudia tukio hilo la kistoria .
Akizungumza na waandishi wa habari  Oktoba 2, 2023 jijini Arusha, Mkurugenzi wa CASSANDRA LINGERIE, ELIFURAHA MLAKI alisema wanayofuraha kumtambulisha mama NAIRO kama chapa ya sura ya biashara yao kwa lengo la kuleta mapinduzi makubwa ya bidhaa zetu na  tunaimani anaushawishi mkubwa wa bidhaa zetu kwa wanawake .
“leo hii Tunayofuraha kumtambulisha balozi wetu MAMA NAIRO katika safari ya kusimamia brand yetu ya CASSANDRA LINGERIE tunaimani  atahamasisha bidhaa zetu kwa wanawake wenzake  kupitia kazi yake ya uchekeshaji wake katika  jamii”
Alisema kwa kweli  tunaimani kubwa na MAMA NAIRO kama chapa ya sura ya bidhaa zao na wamejitolea kuwaletea bidhaa bora wanawake kupitia kauli mbiu yao isemayo mwanamke ni vazi la ndani.
Tunatengeneza wenyewe na kuuza bidhaa zetu kulingana na mahitaji ya mwanamke kuhusu urembo wa vazi la ndani ndio maana tumekuja na MSANII MAMA NAIRO ili kutambulisha bidhaa zetu kwa jamii .

Kwa upande wake wake MAMA NAIRO,ameshukuru kwa Ubalozi huo akidai kwamba huo ni ubalozi wa tatu kulamba  na kueleza kuwa CASSANDRA LINGERIE hawatajutia na maamuzi yao ya kumpatia ubalozi na amejipanga kufanya vurugu zote ili kuwabadilisha wanawake wavae vazi zuri la ndani na kuongeza mvuto kwenye mahusiano.
“Tangu nimeanza kufanya uchekesheji huu ni ubalozi wangu wa tatu ninayofuraha kuwaambia kuwa nitaitendea haki CASSANDRA LINGERIE mpaka mtajuta kunipa ubalozi nitahakikisha kila mwanamke, kila mama na kila msichana anavaa nguo nzuri na bora kutoka CASSANDRALINGERIE”
“Nawataka wanawake wote mniunge mkono ili kuongeza mvuto ndani ya nyumba aina sababu ya mwanaume kuchelewa nyumbani au kwenda kuangalia mpira wakati mwanamke wake muda wote anaonekana mwenye mvuto na mapigo ya kisasa  .
Mwisho