Site icon A24TV News

ANUSURIKA KIFO KWA KIPIGO KUTOKA KWA KATIBU WA MBUNGE NA BABA YAKE MZAZI AMLILIA WAZIRI GWAJIMA KATIBU ATAMBA SIOGOPI CHOCHOTE

 Na Geofrey Stephen ARUSHA 
Wakati Taifa likiadhimisha siku ya mwanamke anayeishi kijijini yanayofanyika  kila mwaka oktoba 15 ,mkazi wa kijiji cha Misigiyo wilayani Ngorongoro Mkoa wa Arusha,Veronica Makutiani(29) mambo yamekuwa tofauti ambapo mwanamke huyo.
amenusurika kuuawa kikatili kwa kipigo cha baba yake mzazi wakishirikiana na kaka yake kiasi cha ujauzito wake kutoka, wakimlazimisha kurejea kwa  mume wake katili aliyekuwa akimtesa kwa kipigo na kumlaza njaa yeye na watoto wake wawili.
Akisimilia mkasa huo kwa uchungu huku akibubujikwa na machozi akiwa amehifadhiwa kwa msamalia mwema Rose Njilo anayefanyakazi shirika la MIMUTIE WOMEN ORGANIZATION la jijini Arusha alisema haamini kama mzazi wake na kaka yake wa damu wanaweza kumfanyia ukatili uliotishia kukatiza uhali wa maisha yake wakimlazimisha kuolewa kwa sababu ya mahali.
Alidai kwamba siku ya tukio oktoba 6 mwaka huu ,baba yake mzazi,Lekerenga Makutiani na Kaka yake Lingato Lekerenga ambaye ni Dereva wa mbunge wa Ngorongoro walimchangia na kumpiga kwa vitu vigumu mpaka akapoteza fahamu wakimshurutisha kurejea nyumbani kwa mume wake, Lesineti Koromo akikokimbia.
Alisema alilazimika kuyakimbia makazi yake alikokuwa akiishi na mume wake kutokana na manyanyaso aliyokuwa akiyapata ikiwemo kipigo ,kushinda na njaa na kunyimwa huduma muhimu kwa madai kwamba amepoteza mvuto baada ya kuzaa.
Alifafanua kwamba aliolewa na mwanaume huyo mwaka 2017 na kubahatika kumzalia watoto wawili lakini katika kipindi chote cha maisha yao ya unyumba maisha yake yalikuwa magumu sana kwani mara nyingi mwanaume huyo amekuwa akimpiga kumnyima chakula na kushindwa kutunza familia yake.
Alisema hivi karibuni mwanaume huyo alimtelekeza na kukimbilia nchini Kenya na kumwachia watoto wake bila msaada wowote wa chakula hali iliyomlazimu kushinda njaa na kumlazimu kurejea nyumbani kwa wazazi wake.
“Baada ya kufika nyumbani kwa wazazi wangu nikiwa nimedhoofu sana mimi na watoto wangu wawili ,baba yangu alinifukuza na kuniambia nisikae hapo niondoke na nirudi kwa mume wangu”
“Nilikataa kuondoka nikamweleza hali halisi ya nyumbani kwangu na mateso ninayoyapata nikimweleza simtaki tena huyo mwanaume ananitesa sana ,baba yangu na kaka yangu walikataa na kuniambia niondoke hapo vinginevyo wataniua na hawatakuwa na chakupoteza”
Alisema siku hiyo aliamua kuondoka na kwenda kuomba hifadhi ya kulala kwa watu baki na kesho yake alionekana akiranda randa kijijini hapo ndipo kaka yake alipomfuata na kuleta nyumbani na kuanza kumpiga kwa vitu vigumu huku wakimchangia kwa kipigo na baba yake alikuwa akimkanyaga tumboni na kwenye mbavu na damu zikaanza kumtoka sehemu za siri akapoteza fahamu.
“Wakati wakinipiga mama yangu alikuwa akilia kwa uchungu lakini hakuwa na namna yoyote ya kunisaidia kutoka na mfumo dume wa mwanamke kutosikilizwa”
Alisema akiwa hajitambui na akiwa ametelekezwa nje ua nyumba majira ya usiku mama yake alikuja na kumchukua na kuanza kumpatia huduma ya dawa za kimasai ndipo alipozinguka na siku ya tatu wasamalia wema walimwona na kumpeleka katika zahanati iliyopo kijijini hapo kwa ajili ya matibabu.
Amemuomba waziri Dorth Gwajima kumsaidia kwani mpaka sasa atambui watoto wake wakonkatika hali gani ya maisha
Mganga mfawidhi wa zahanati hiyo Samweli Panga alipohojiwa na gazeti hili alikiri kumpokea Veronica akidai kwamba alifikishwa katika zahanati hiyo na watu waliodai ni wasamalia wema.
“Baada ya kumpatia vipimo tuligundua kwamba alikuwa na majeraha na uvimbe kichwani na alikuwa akilalamika mbavu kuuma na maeneo mengine ya mwili yanayoinesha alishambuliwa ,tulimtundikia drip chupa tatu na baadaye hali yake ilipotengamaa  tulimruhusu kwa kumkabidhi kwa mtendaji wa kata hiyo”
Naye mtendaji wa kata ya Misigiyo, Onesmo Munga alisema alipata taarifa za tukio hilo na kufika katika zahanati hiyo na baadaye walifanya utaratibu wa kuokoa maisha yake kwa kutafuta msaada wa kujikimu ndipo walipomsafirisha hadi mjini Arusha na kumpatia hifadhi wakati taratibu zingine zikiendelea.
Kwa upande kwake Rose Njilo mratibu wa shirika la Mimutie Women Organization  alisema ,alipokea taarifa za Veronica kutoka kwa afisa mtendaji wa kata hiyo na alimpokea nyumani kwake akiwa na hali mbaya na alipo mhoji alidai amepigwa na baba yake pamoja na kaka yake wakimlazimisha kuolewa.
Alisema shirika hilo litahakikisha linasimamia haki za mwanamke huyo iliwemo wahusika kuchukuliwa hatua kwa sababu anajua familia za kifugaji
“Sisi kama taasisi tunapambana na haki  ya mwanamke kuhakikisha  inapatikana na wahusika wa matukio ya ukatili na unyanyasaji wanachukuliwa hatua za sheria “
Kwa upande wake Katibu wa mbunge Lingato Lekerenga alipohojiwa kwa njia ya simu alikiri kumshambulia kwa kipigo dada yake akishirikiana na baba yake akidai ni utaratibu wa mila zao kutoa adhabu hiyo pale inapobainika mhusika wa damu wamekosea.
“Ni kweli Veronica ni dada yangu tena nampenda sana na nikweli nilimpiga ila nilimpiga kidogo tu kwa sababu alitukosea heshima kwa kukataa kwenda alikokuwa ameolewa”
Alisema kwa sasa yupo tayari kumwomba masamaha ili yaish2 na aje kuishi nyumbani mpaka hapo mambo yake ya ndoa yatakapokaa sawa yeye ba mme wake.
Jitihada za  kumpata kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Justine Masejo ili kuzungumzia suala hilo hakuweza kupatikana .
Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Raymond Mangwala alipoulizwa kwa njia ya simu iwapo anataarifa za tukio hilo alisema hana taarifa ndo amefanyakuzikia kwa mwandishi wa habari.
Hata hivyo aliahidi kufuatilia ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
Ends