Site icon A24TV News

WACHIMBAJI WA MADINI CHANGAMKIENI FURSA YA MAONESHO KUTAKA BIMA

Na Richard Mrusha Geita

WACHIMBAJI mbalimbali wa madini nchini wameshauliwa kukatia bima mitambo wanayotumia katika shughuli zao za uchimbaji ili pale inapotokea imeharibika ili waweze kutengenezewa bila kuathiri shughuli zao za uchimbaji.

Akizungumza katika maonesho ya sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya EPZA Bombambili halimashauri ya mji Geita.

Meneja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) kanda ya ziwa
Stella Marwa amesema kuwa bado kumekuwa na muamko wa ukataji bima kwa upande wa wachimbaji ambapo ametoa rai kwa wachimbaji hao kuchangamkia fursa hiyo kutokana umuhimu wa bima hiyo.

Aidha ameongeza kuwa katika maonesho hayo pia wameenda kutoa pia kuhusu ukataji wa bima ya maisha wachimbaji kukata bima ya ajali ambayo itamsaidia mchimbaji pale ambapo anaweza kupata madhara katika shughuli zake za uchimbaji hivyo hao kama NIC kupitia bima yake ya ajali kwa ajili ya wachimbaji itaweza kumrudisha katika hali yake ya kawaida na endapo itatokea bahati mbaya amefariki warithi wake wanaweza kufidiwa na kuendeleza shughuli zao zakiuchumi.

Ameongeza kuwa mbali kutoa bima elimu ya bima hizo pia wanatoa elimu ya bima ya maisha ambayo ina uwekezaji ndani na ulinzi ndani ambayo inamhakikishia mchimbaji au mtu ²mwingine yeyote kuwa ukipatwa na janga lolote lile familia ikiwemo watoto wataendelea kusoma.

“Pia katika maonesho haya tumekuja kutoa elimu kwa watumiaji wa vyombo vya moto kama magari,pikipiki na bajaji tunatoa elimu hii ili hao wasafirishaji waweze kukata bima hizo na kuepusha ajali ambazo zinaweza kuwatokea ikapelekea hayo magari yao kutokutengenezeka kabisa sababu yakutokuwa na bima wakikata bima na NIC Insurrance tutawalipa ndani ya siku saba na taratibu zote tunafanya kulingana na miongozo na zakumkatia ndiyo maana tunalipa ndani ya siku saba”amesema Marwa.

Aidha ameongeza kuwa NIC wameweza kufanya mabadiliko makubwa kwa kipindi kifupi ambapo wanatembea kifua mbele kuwa wana uwezo wakulipa madai ndani ya siku saba.

Aidha ametoa wito kwa wakazi wa Geita katika kipindi hiki cha maonesho kutembelea banda hilo kupata elimu mbalimbali kuhusu bima.

Mwisho