Site icon A24TV News

TEA ITAENDELEA KUTOA UZOEFU KUBORESHA UZALISHAJI WA VIUATILIFU NA KUPAMBANA NA VISUMBUFU VYA MAZAO NCHINI KWA KUSHIRIKIANA NA COSTECH

Na Ahmed Mahmoud
Umoja wa Wanasayansi ya Udhibiti wa Wadudu waharibifu wa Mazao nchini(TEA) umeeleza utaendelea kufanya utafiti zenye kuleta matokeo sahihi ya kukabiliana na Wadudu waharibifu ambao wanaleta athari kwa Afya za binadamu wanyama na Mazingira.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania TPHPA Prof.Joseph Ndunguru katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wanasayansi waudhibiti wa visumbufu vya Mazao unaofanyika Jijini Arusha.
Amesema kwamba uwepo wa majadiliano ya tafiti utasaidia kuongeza tija na kuboresha uzalishaji wa mifugo Mazao na hivyo kuongeza soko na usalama wa chakula nchini.
“Mkutano huu ni Jukwaa la kuona umuhimu wa tafiti zetu za Mazao na Viuatilifu zinapata nafasi ya kuongeza uzalishaji wenye tija sanjari na kupata uzoefu kwa wanasayansi ili kuboresha na kuondoa changamoto ya visumbufu vya Mazao”
Awali Mwenyekiti wa Umoja wa
Wanasayansi waudhibiti wa visumbufu vya Mazao TEA Prof. Gration Rwegasira amesema kwamba Mkutano huo ni Jukwaa la wanasayansi kujenga mahusiano kwa kuchanganya uzoefu tafiti na bunifu kwa Lengo la kuboresha Viuatilifu vya Mazao kuleta tija ya uzalishaji.
Amesema kwamba walipokutana ni wanasayansi ya Wadudu kwa ajili ya kuangalia namna Bora ya kudhibiti Wadudu waharibifu na kutunza Wadudu wenye kuleta faida katika Mazao ili kutunza mazingira.
Kwa Upande wake Mwakilishi Kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH Dkt.Deogracious Protas amesema COSTECH itaendelea kushirikiana na kuwezesha watafiti kubuni na kufanya tafiti mbalimbali kwa kutoa fedha kuboresha ili kuongeza tija ya maendeleo ya tafiti nchini.
Amesema kwamba Serikali kupitia COSTECH imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya Tafiti ndio maana wameshiriki Mkutano huo kwa Lengo la kuendeleza tafiti za Mazao na Viuatilifu sanjari na kupambana na visumbufu vya Mazao.
Hata hivyo Mmoja ya Wanachama wa Umoja huo kutoka chuo cha COHAS Muheza Dr. Elison Kemibala amesema kwamba Umoja huo ni nguzo muhimu sana katika mnyororo wa thamani ya Mazao katika kupambana na visumbufu vya Mazao Mifugo na Afya ya binadamu iliyotokana na madhara ya wanyama.
Alisema Muingiloano wa magonjwa ya binadamu na wanyama ni sehemu ya kuangalia sana ili kuleta tija na uzalishaji wa Mazao ya mifugo kilimo na wanyama sanjari na kuboresha mazingira hapa nchini.
Mwisho .