Site icon A24TV News

TAARIFA FUPI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO NA SHUGHULI ZA SERIKALI KIPINDI CHA JULAI HADI SEPTEMBA,2023 KATIKA JIJI LA ARUSHA

 

Na Mwandishi wa A24A24Tv

Katika Mwaka wa fedha 2023-2024 Halmashauri imeendelea kusimamia na kutekeleza miradi mbali mbali ya Maendeleo na shughuli za serikali kupitia Mapato ya ndani na Ruzuku ya serikali kwa fedha zilizotolewa mwaka 2022-2023 na fedha za Mapato ya ndani zilizotolewa Mwaka 2023-2024. Shughuli na majukumu mbalimbali yamesimamiwa na kutekelezwa kama ifuatavyo:

Ujenzi wa ofisi za Kata Sakina na Osunyai umekamilika bado uwekaji wa samani mpya. Ofisi ya Kata Osunyai wamepatiwa fedha za uwekaji samani Tshs 3,000,000.00 zilizotolewa Mwezi Juni,2023. Ofisi ya Kata ya Moivaro Inaendelea na ujenzi, imepauliwa, kwa sasa inaendelea kupigwa ripu, ‘’blundering imefanyika, ‘’grill za madirisha zimewekwa, mabomba ya mfumo wa umeme yamewekwa, taratibu za manunuzi zinaendelea kwa ajili ya uwekaji vigae na kazi nyingine za ukamilishaji.

Ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi, iko hatua ya ukamilishaji, vigae vinamaliziwa kuwekwa, uzio umejengwa bado lipu, rangi imepakwa, kibanda cha mlinzi kimejengwa bado kupauliwa. Taratibu za manunuzi zinaendelea kwa ajili ya upachikaji milango na ukamilishaji.

Jengo la Makao Makuu ya Halmashauri, mtaalamu mshauri anaendelea na kazi, mchakato wa kupata mkandarasi ulifikia hatua ya mwisho, kutokana na changamoto ya mchakato kutozingatia baadhi ya taratibu za msingi, Uongozi wa Mkoa umeagiza mchakato urudiwe upya ili kupata mkandarasi wa ujenzi. 

 

Tangazo litatangangazwa kwenye mfumo mpya wa ununuzi wa NEST ifikapo mwezi Oktoba.

 

Ukarabati wa Soko kuu na soko la Kilombero umefanyika kwa kuweka paa baadhi ya maeneo yaliyokuwa na uhitaji wa ukarabati,  mitaro imejengwa soko la Kilombero na Samunge. Katika mwaka huu wa fedha 2023/2024 ukarabati zaidi utafanyika soko kuu, soko la Kilombero, soko la Samunge, soko la Mbauda, Lemara na masoko mengine.

Ofisi ya machinga imekamilishwa soko la ulezi, ujenzi wa soko la machinha unatarajiwa kuanza mwezi Oktoba kutokana na kuisha kwa changamoto ya umiliki wa ardhi ya eneo la ujenzi.

 

Changamoto ya mradi wa viwanja eneo la Bondeni city imekamilika na viwanja vimeuzwa mwezi wa nane(Agosti). Miradi yote inayohusiana na mradi wa Bondeni city inatarajiwa kuendelea na utekelezaji ikiwamo ujenzi wa stendi ya kisasa ya mabasi ya kwenda Mkoani.

 

 

 

Kupitia mradi wa BOOST, ujenzi wa shule mpya ya mikondo miwili imejengwa eneo la Msasani, madarasa 23 yamejengwa, madarasa manne(4) ya mfano 

 

kwa ajili ya elimu ya awali yamejengwa, darasa la wanafunzi wenye mahitaji maalum limejengwa na vyoo matundu 45 vimejengwa na kukamilika.

 

Shule mpya ya msingi eneo la Korongoni Kata ya Lemara unaendelea kupitia mapato ya ndani, madarasa manne ya chini yamekamilika. Vyoo matundu 11 vinaendelea kukamilishwa, madarasa manne(4) na vyoo matundu 11 kwa ghorofa ya kwanza yanaendelea kujengwa. Halmashauri kupitia mapato ya ndani imetoa Tshs 365,000,000 na serikali kuu imetoa Tshs 400,000,000.00. Shule hii inatarajiwa kukamilika mwezi Desemba,2023 na kuanza kupokea wanafunzi mwezi Januari,2024.

Shule nyingine mpya ya ghorofa ya msingi inayojengwa eneo la NAFCO mkandarasi amepatikana na ujenzi unatarajiwa kuanza wakati wowote.

Aidha Halmashauri kupitia mapato ya ndani imekarabati madarasa shule za msingi Levolosi, Kaloleni, Kijenge, Sanawari, Sombetini, Sokoni I, Moshono, Wema nk. Madarasa manne(4) ya ghorofa ya chini na jengo la Utawala shule ya Msingi Murriet Darajani yanatarajiwa kukamilishwa kabla ya mwezi Novemba na fedha imeshapelekwa katika shule husika.

Kupitia mradi wa TASAF uzio umejengwa SM Shangarao.

Katika mwaka huu wa fedha 2023-2024 madarasa yataendelea kukarabatiwa, madawati zaidi yatatengenezwa na miundombinu zaidi katika shule mpya zinazojengwa ikiwamo majengo ya utawala, madarasa na vyoo yataendelea kujengwa.

 

Shule mpya ya sekondari  ya ghorofa iliyojengwa kwa mapato ya ndani na mradi wa SEQUIP imekamilika kwa miundombinu ya awali na kusajiliwa(Murriet Mlimani), na walimu na wanafunzi wameshapangiwa. Serikali imeshatoa fedha ya ujenzi wa nyumba ya walimu. Ujenzi utaanza wakati wowote.

Shule mpya ya sekondari ya Kata ya Sekei inaendelea kujengwa eneo la shule ya msingi Kijenge. Baadhi ya majengo kuta zimeanza kujengwa na mengine yako hatua ya msingi.

Uboreshaji wa miundombinu kwa kujenga miundombinu mipya shule za sekondari za kidato cha tano inaendelea na ujenzi.

 

Shule ya sekondari Korona mabweni manne(4), madarasa 11 na matundu ya vyoo 16 yamekamilika kujengwa. Bweni lingine jipya la 5 linaendelea na ujenzi kwa kuwa fedha yake imetolewa mwezi wa nane kupitia fedha za ruzuku ya serikali. Kupitia mapato ya ndani mabweni mawili(2) yamekamilishwa na bwalo la chakula linaendelea kukamilishwa.

Shule ya sekondari ya wasichana Arusha madarasa 15, mabweni 2 na matundu ya vyoo 21 yanaendelea na ujenzi kupitia Mpango wa serikali kwa fedha za Barrick.

Kuptia mapato ya ndani vyoo vya wanafunzi na walimu shule za sekondari Kaloleni na Njiro vinaendelea na ujenzi. Uzio shule za sekondari Arusha Terrat na Kaloleni unaendelea kujengwa.

Madarasa manane ya ghorofa yamejengwa na kukamilika shule ya sekondari Arusha Terrat.

Kupitia mapato ya ndani mwaka huu 2023/2024 mabweni mawili na bwalo la chakula shule ya sekondari Mrisho Gambo yameshapelekewa fedha kwa ajili ya ukamilishaji. Halmashauri imetoa Tshs 160,000,000.00

Utengenezaji viti na meza utaendelea

 

Jengo la OPD hospitali ya Halmashauri linaendelea na ujenzi, kwa sasa maandalizi ya kumwaga ‘’slab’’ yanafanyika kwa kujenga miundombinu ya umwagaji zege.

Zahanati ya Orkereyan imekamilka na inaendelea kutoa huduma.

Kituo cha Afya Mkonoo kimekamilika na kinaendelea kutoa huduma.

Jengo la mama na mtoto zahanati ya Sombetini limeshapelekewa fedha kwa ajili ya kukamilisha uwekaji wa milango iliyobaki ili lianze kutoa huduma.

Jengo la mama na mtoto kituo cha Afya Moshono liko hatua za mwisho za ukamilishaji, Halmashauri kupitia mapato ya ndani imeshatoa Tshs 130,000,000.00 kwa mwaka 2022/2023.

Jengo la upasuaji kituo cha Afya Moivaro litaanza kujengwa wakati wowote halmashauri imeshapeleka fedha kupitia mapato ya ndani Tshs 70,000,000.00

Jengo la wagonjwa wa nje la ghorofa kituo cha Afya Daraja II litaanza kujengwa kabla ya mwezi Desemba,2023 Halmashauri inapeleka Tshs 200,000,000.

 

Zahanati ya Maweni inatarajiwa kukamilika na kuanza kutumika kabla ya mwezi Desemba,2023. Halmashauri kupitia mapato ya ndani imetenga fedha za ukamilishaji.

Kituo cha Afya Levolosi mkandarasi ameshapatikana na amekabidhiwa eneo la mradi na ujenzi wa jengo la OPD maandalizi ya mkandarasi kuendelea na ujenzi yanaendelea kufanyika.

Uboreshaji wa vifaa tiba unaendelea kwa kununua vifaa vipya vituo vya Afya Moshono, Mkonoo na zahanati za Baraa.

 

Wakati tunasubiri maelekezo ya serikali kuhusu utaratibu mpya wa utoaji mikopo ya vikundi Halmashauri inaendelea kutenga fedha ya asilimia 10 kupitia mapato ya ndani kila makusanyo yanapoendelea. Kwa mwaka huu zimetengwa fedha za mikopo zaidi ya billioni nne.

 

Kupitia mapato ya ndani kazi ya uwekaji wa taa za barabarani inaendelea kufanyika na ukarabati wa barabara kupitia wakandarasi na bara bara zilizoainishwa unaendelea kufanyika kwa mikataba yam waka 2022/2023.

Na mwaka huu wa fedha kama ilivyo utaratibu Halmashauri imetenga fedha zaidi ya billioni nne(4,000,000,000.00) kwa ajili ya kazi za barabara.

 

Pamoja na miradi hii ya miundombinu, Halmashauri inaendelea kuimarisha mikakati ya ukusanyaji mapato ya ndani na usimamizi wa fedha za umma.

 

Halmashauri inaendelea kuimarisha utawala bora kwa kuitisha vikao vya kisheria na kulipa stahiki za watumishi na Waheshimiwa Madiwani

Naomba kuwasilisha

 

Inj,Juma Hamsini

MKURUGENZI WA JIJI

ARUSHA