Site icon A24TV News

SERIKALI YA AWAMU YA SITA YALETA KICHEKO KWA WACHIMBAJI MABEKI YAAITIKIA KUTOA MIKOPO

Na Richard Mrusha Geita

WAZIRI WA Madini Antony Mavunde amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan iko katika mazungumzo baina ya wizara ya Madini na Tanzania Banker’s Association, taasisi zote za fedha (MABENKI), STAMICO na wadau wa sekta Madini kujadiliana ili kuona ni changamoto gani zinazosababisha mchimbaji wadogo wa Madini wasiwe na vigezo vya kuweza kupewa mkopoo.

Hayo ameyesema Leo Alhamis September 28,2023 katika kongamano la kujadiliana fursa zilipo Geita pamoja na “Local Contect” kwenye Maonesho ya sita sita ya kimataifa ya teknolojia ya Madini yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZA bombambili halmashauri ya mji Geita.

Akizungumza mbele ya wachimbaji wadogo wa Madini Waziri wa Madini Mavunde amesema”Mnamo tarehe Tano mwenzi wa kumi mwaka huu tutakuwa na kikao Cha siku nzima kuzungumza na wenzetu wa Tanzania Banker’s Association na Taasisi za kibenki kujadiliana ni kwa namna gani mchimbaji mdogo wa Madini ataweza kupewa mkopo na pia ,Wao kama wachimabji waya mda wakuongea changamoto zao zinazosababisha mchimbaji mdogo wa Madini asiwe na vigezo vya kuweza kupewa mkopo,Hivyo sisi wizara ya madini tutazichukua hizo changamoto tutazijadili hizo changamoto kwa pamoja na kupata majibu,”amesema Mavunde.

Aidha, Waziri wa Madini Mavunde amewahakikishia na kuwaahidi wachimbaji wadogo wa Madini kwamba hivi karibu wataanza kukopesheka kutoka taasisi za kifedha (MABENKI) amesema “Naomba niwahakikishie wachimbaji wadogo wa Madini mara baada ya kikao hiki kinachotarajiwa kufanyika tarehe Tano mwenzi wa kumi mwaka huu Jijini Dar es salaam tutuanza kupokea mikopo kutoka taasisi za fedha kwa ajili ya mitaji katika shughuli zetu za uchimbaji.

Amesema anawapongeza wadau wa sekta ya madini kwa kutekeleza wazo la kufungua Benki ya wachimbaji Madini,ambapo wameweza kujichangisha wenyewe mtaji na kupatika kiasi Cha pesa za kitanzania Billion Mbili ambazo zimetoka mifukoni mwao,Nawapongeza kwa Hilo mmeonyesha kwa kuwa Madini ni Maisha na utajiri.

Mwisho