Site icon A24TV News

LISU AMALIZA MAHOJIANO KITUO CHA POLISI ARUSHA MIKUTANO IKO PALE PALE NGORONGORO NA KARATU

Na Geofrey Stephen Arusha .

Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa,Tundu Lissu amezungumza na vyombo vya Habari mara baada ya kumaliza mahojiano na jeshi la polisi Mkoani Arusha na kudai amehojiwa kuhusu kufunga barabara ambapo alikanusha madai hayo kwa kile  alichoeleza kuwa yeye alikuta barabara hiyo imeshafungwa na polisi waliovaa kiraia wakilenga kumzuia asiende kwenye mikutano yake Ngorongoro.

Lissu amesema mikutano yake katika Jimbo la Ngorongoro iko pale pale pamoja na karatu itafanyika mara baada ya mapumziko ya siku chache  hivyo wananchi wavute subira watatangaziwa siku na wapi mikutano itafanyika tena .

amesema vibali vya kufanya mikutano Ngorongoro avitoki kwa jeshi la polisi na walisha maliza taratibu zote kutoka kwa mamlaka ya Ngoro ngoro  hivyo wananchi wasiwe na ofu kwamba mikutano aita fanyika tena kwa kikwazo cha vibali kutoka kwa jeshi la polisi,

Mwisho