Site icon A24TV News

JAMII YAASWA KUTUNZA MAZINGIRA KWA KUPANDA MITI

Na Richard Mrusha Geita

MKURUGENZI wa Kampuni ya Ruth Bertha Supply Ruthberth Myonga amesema kuwa ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi Kuna umuhimu wa kuhakikisha kila Mtanzania anashiriki kikamilifu upandaji miti ikiwa pamoja na kuunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na wadau wa Mazingira.

Hayo yamesemwa leo Septemba 22 Mwaka huu Mkoani Geita na Mkurugenzi wa Ruthberth ,Ruthberth Myonga kwenye Maonyesho ya sita ya kitaifa ya Teknolojia Madini yanayofanyika katika Viwanja vya Bombambili .ambapo pia amewahamasisha wanawake kote nchini kupanda miti mbalimbali ya matunda na kivuli Kwa lengo la kudhibiti mabadiliko ya tabia ya nchi.

Amesema kuwa mbali na kupanda miti ya matunda pia wajikite katika kupanda miti ya maua na hiyo ni kutokana na Fursa inayopatikana katika miti ya maua ambapo itawasaidia kujikwamua kiuchumi .

” Ruthberth Kampuni tupo katika Maonyesho haya lengo kubwa nikuja kuwahamasisha Watanzania juu ya umuhimu wa kupanda miti na kutunza mazingira na ikimbukwe kuwa hivi Sasa Kuna changamoto kubwa ya mabadiliko ya tabia nchi hivyo ni muhimu Kwa kila Mtanzania kupanda na kutunza Mazingira kwenye maeneo yanayozunguka “amesema.

Nakuongeza kuwa ” hivi Sasa katika mikoa ya Kanda ya ziwa ikiwemo Mkoa huu wa Geita kumekuwa na muamko mkubwa wa watu kupanda miti ya matunda na hata hapa mmeona watu mbalimbali wanakuja kuuliza na kununua miti kwani wamejua umuhimu wa kupanda miti nakwamba tunahamasisha zaidi kupanda miti ya matunda ,miti dawa, na miti ya kivuli.” Amesisitiza

Ruthberth pia ametoa shukrani zake Kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Mazingira Kwa kuwaunga mkono juhudi zinazofanywa na wadau ikiwa pamoja na kutoa matamko mbalimbali yanayohamisisha upandaji wa miti na kupitia Kampuni yake watahakikisha wanaongeza kasi ya kuelimisha Watanzania pamoja na kuzalisha miti Kwa wingi ili kila Mwananchi apande miti hiyo .

Ameongeza kuwa wao kama Kampuni licha ya kuwataka Watanzania kupanda miti lakini pia wanahakikisha wanafuatilia ili kupata taarifa zake Kwa lengo la kuona miaka 200 ijayo itakuwa imepunguza kasi ya ukataji miti hivyo anawaalika wakazi na wananchi wa Mkoa wa Geita kutembelea katika Banda lake ili kuona aina mbalimbali za miti ukiwemo ukwaju wenye Radha kama ya tende ambao pia unatiba ndani yake na mapera mekundu ya kilo Moja ambayo mbegu yake ni endelevu.

Wakati huohuo Mkurugenzi huyo ametoa ushauri Kwa waau mbalimbali ambao wanaomba fedha Kwa ajili ya Mazingira kuhakikisha fedha hizo zinatumika kwenye eneo lililokusudiwa na si kufanya ujanjaujanja kwani kufanya hivyo nikurudisha nyuma harakati za Serikali ya awamu ya sita ya Rais DKT.Samia Suluhu Hassan ambayo inahamasisha uutuzaji wa Mazingira,kupanda miti katika maeneo mbalimbali nchini.

Mwisho