Site icon A24TV News

GEUWASA YAJINASIBU KUMALIZA TATIZO LA MAJI GEITA MJINI.

Na. Costantine James , Geita.

Mamlaka ya Maji na Usafi na Mazingira mjini Geita imesema imeandaa mikakati Madhubuti kuhakikisha miradi inayoendelea kutekelezwa na ijayo inakamilika kwa wakati uliopangwa Ili kuhakikisha kuwa wanatatua Changamoto ya upatikanaji wa Maji safi na salama kwa wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Geita.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa GEUSA Mhandisi Frank Changawa wakati akielezea mipango na mikakati mbele ya Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini alipotembelea banda la GEUWASA kwenye maonyesho 6 ya Teknolojia ya madini yanayofanyika Mjini Geita amesema kwa Sasa Maji yanatoka kwa mgao lakini miradi mingi inatekelezwa ukiwemo ule wa miji 28 ambao unatarajiwa kukamilika oktoba 2025 ambao utaondoka kabisa tatizo la Maji safi na salama.

Amesema kwa Sasa Mji wa Geita unahitaji Maji Lita Milioni 20 kwa siku pindi mradi wa chujio la nyakanga utakapokamika mwishoni mwa mwezi oktoba utasogeza mbele upatikanaji wa Maji kutoka Lita Milioni 4 inayopatikana kwa sasa mpaka Lita Milioni 7 kwa siku.

 

Aidha kwa upande Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Constantine Kanyasu amewaomba mamlaka hiyo kumalizia miradi hiyo kwa wakati Ili kutimiza adhma ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani ya kumtua mama ndoo kichwani

Mwisho .