Site icon A24TV News

GAVANA BOT AWATAKA WACHIMBAJI KUTOTEMBEA NA FEDHA TASLIM

Na Gift Thadey, Geita

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Emmanuel Tutubaamewasihi wachimbaji wa madini nchini kutotembea na fedha taslim mifukoni badala yake watumie mifumo ya kielektroniki katika kutoa na kupokea fedha.

Gavana Tutuba ameyasema hayo Mjini Geita wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya sita ya kimataifa ya teknolojia ya madini.

“Nawashauri wachimbaji kutumia mifumo ya kielelektoniki kupokea na kutoa fedha badala ya kutembea na fedha taslimu,” amesema Tutuba.

Gavana Tutuba amesema wao kama BOT wanalipa kwa mfumo wa TIPS ambao unarahisisha kwa kuwa umeunganishwa na mabenki yote na miamala ya simu nchini.

“Ndiyo sababu tunawahamasisha watumie mifumo ya kielektroniki kuliko fedha taslimu kwa kuwa ni mfumo wa haraka na una nafuu utawaepusha na fedha bandia,” amesema Gavana Tutuba.

Amesema kuwa na mfumo wa kielektroniki ni nafuu zaidi hata kuepuka kuibiwa fedha tofauti na kuwa na fedha taslimu mkononi au mfukoni.

Mwisho.

MWISHO