TIMU za kusimamia hospitali za rufaa Nchini zimesisitizwa kuhakikisha kwamba zinasimamia ipasavyo  utendaji wa timu za uboreshaji wa huduma za  afya ngazi za mikoa na Wilaya ili kupatikana huduma bora kwa wananchi.

 
Msisitizo huo umetolewa Leo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,John Mongela,alipokuwa akifungua mafunzo ya wiki mbili ya timu za usimamizi na uendeshaji huduma za afya hospitali za Kanda Nchini yanayofanyika kwenye Kituo cha maendeleo ya Elimu ya afya CEDHA,Jijini Arusha.
Mongela,alisema kuwa  Katika kipindi cha miaka miwili Serikali imefanya uwekezaji mkubwa sana kwenye vifaa na miundo mbinu ya afya 
hivyo ametaka timu hiyo kuhakikisha kuwa mafunzo wanayoyapata yanawezesha kutoa huduma kwa kiwango  kinachotarajiwa.
Aliwataka wakaboreshe utendaji ili kuondoa mapungufu na waimarishe usimamizi Kwa kuzijengea uwezo timu za mikoa na Wilaya na baada ya mafunzo hayo  hategemei kuona mapungufu Katika utoaji huduma za afya Kwa wananchi
Naye Mkurugenzi Msaidizi  Tiba na Utafiti kutoka wizara ya Afya,Luteni Kanali Dkt Pius Kabusubuto,Kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya afya,alisema kuwa Wizara inafanya kazi kuhakikisha agenda ya Rais Samia ya Kutolewa huduma bora Kwa wananchi inatimia.
 
Dkt Kabuzubuto ambae ni mratibu wa mafunzo hayo alisema kuwa Rais ,ametoa shilingi bilioni 264  Kwa Wizara ya afya Kwa ajili ya Uwekezaji wa miundo mbinu,ununuzi wa vifaa tiba,mafunzo kwa madaktari bingwa na mabingwa wabobezi  ili kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda nje ya nchi Kwa matibabu zaidi.
Alisema ili kupata  matokeo makubwa  ya Uwekezaji huo kinachotarajiwa ni yale yanayotokea kwenye hospitali na Vituo vya afya  yawe na kasi
Awali Mkuu wa Taasisi hiyo ya maendeleo ya Elimu ya watumishi wa Afya Arusha (CEDHA),Dkt Johannes Lukumay alisema kuwa kupitia Shirika la misaada la kimataifa la Japan,JICA,Kituo hicho Cha CEDHA, kitakuwa kikubwa na kinaanza kutoa mafunzo hayo ya Uongozi na usimamizi wa huduma za afya kwa nchi Afrika zinazozungumza lugha ya Kiingereza 
Dkt Lukumay ambaye pia ni mratibu wa mafunzo hayo alisema hiyo ni heshima Kwa taifa ambayo imetolewa kwa taasisi hiyo lengo la mafunzo hayo ni  uboreshaji  wa huduma na  utoaji wa mafunzo ya msingi yanauohusu utawala ili kudumisha stadi za Uongozi .
 
Alisema kuwa Serikali ya Japan,imeelekeza kuwa mafunzo hayo yataanza Kutolewa CEDHA na hivyo Viongozi waliokuwa wakipelekwa Japani Kwa mafunzo hayo sasa watayapata hapa Nchini 
 
Alisema kuwa Taasisi hiyo iliyoanzishwa mwaka 1983 imepewa jukumu kubwa la kuratibu shuguli zote za mafunzo zinazohusisha utawala na Uongozi kwa Sekta ya afya Nchini.

Mwisho .