Site icon A24TV News

TCCIA WAENDESHA MAFUNZO KWA WAJASIRIA MALI VIJANANA KINA MAMA ,NA WENYE ULEMAVU

Na Geofrey Stephen Arusha .

Chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo TCCIA, kimetoa  mafunzo ya uhusishwaji wa kibiashara kwa wamachinga,vijana, wamama wa sokoni na watu wenye ulemavu.

Akifungua mafunzo hayo Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Maxmilliane Iranghe, amesema jiji la Arusha litatoa mikopo isiyokuwa na riba na riba nafuu kwa akina mama, vijana na watu wenye ulemavu”

Amesema Jiji la Arusha Tumetenga takribani shilingi Billioni 4, Ela hii ikienda kwenye mzunguko itawatoa wafanyabiashara mahali walipo kwenda sehemu wanapotaka kufanya biahara .

Mstahiki Meya amehasa makapuni mengi kuendelea kuandaa mafunzo kwa wajasiriamali kwa kuwapatia elimu itakayowainua kibiashara ilikuendelea kutengeneza wafanyabiashara wengi na wakubwa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa TCCIA Arusha,Walter Maeda amesema kuwa wameaanda washa hiyo ilikuwapa motisha wafanyabiashara wadogo na wamachinga kuweza kufanya kazi kwa kujiamini na kufanya biashara katika mazingira ya usafi.

Amesema  kuwa kila mfanyabiashara anapaswa kujijenga vizurii katika mazingira yake ya kazi na kuwa na vitambulisho maalum iliviweze kuwasaidia wao kutambuliwa na jiji la Arusha wakiwa kama wafanyabiashara iliwaweze kupata mikopo nafuu kwaajili yakuendeleza biasharaa zao.

Afisa biashara wa Shirika hilo Charles Salvatory, amesema wameaanda mpango huo wa mafunzo kwa wakinamama wajasiriamali ilikuweza kujua ni kwanamna gani wanaweza kuendesha biashara zao kwa kisasa zaidi”

Tuna mpango wakuwawezesha kiuchumi kupitia mikopo yenye riba nafuu na kuwakutanisha na wafanyabiashara mbalimbali “alisema Bwana Makoi.

MWISHO.