Site icon A24TV News

TARURA RUANGWA YATEKELEZE UJENZI WA BARABARA ZA MIGODI KWA SH BILIONI KUMI NA MOJA

Na Richard Mrusha Ruangwa

ZAIDI ya shilingi bilion kumi na moja zimetumika katika mwaka wa fedha 2021/2022 katika ujenzi wa barabara zinazoelekea katika maeneo migodi Wilayani Rwangwa mkoani Lindi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya madini yanayoendelea katika wilaya ya Rwangwa ,Meneja Tarura Wilaya ya Rwangwa Mashaka Narubi amesema kuwa pia mwaka huo huo wa fedha 2021/2022 wamejenga barabara za lami maeneo ya mji wa Rwangwa mjini ambazo zinaelekea maeneo yote ya migodi ambapo zimegharimu shilingi bilioni 5.2.

Amesema lengo la ujenzi wa barabara hizo ni kurahisisha shughuli za uchimbaji wa madini unaoendelea Wilayani humo ili ziweze kupitika katika kipindi chote cha mwaka.

“Kwenye mpango wetu wa mwaka 2021 mpaka mwaka 2023 tumejenga jumla ya madaraja madogo 47 ambapo shilingi bilion 1.5 zilitumika katika ujenzi huo na madaraja yote tuliyoyajenga maeneo ya vijijini ambapo ni kama fursa kwa wachimbaji wetu wa madini”amesema mashaka.

“Mwaka huu wa fedha 2023/2024 tunakusudia kujenga barabara kilomita 110 kuelekea maeneo ya madini ambapo tunatarajia kutumia bilion 3.4 kwa ajili ya barabara katika maeneo ya madini”ameongeza.

Pia amesema Tarura Wilaya ya Rwangwa imejikita zaidi kuboresha barabara zinazoelekea kwenye maeneo yenye fursa ya madini ambapo wanaamini kwakufanya hivyo wawekezaji wa madini watajitokeza kwa wingi wilayani humo.

Mashaka ameongeza kuwa mbali na kujenga barabara hizo pia wana mpango wakuongeza barabara nne ambazo zitaelekea kwenye maeneo ya madini kwa kiwango cha lami kutoka Rwangwa kuelekea eneo la Nangurugai ambapo kuna mgodi wa grafact ambapo amesema wameshaanza usanifu na mwezi wa kumi mwaka huu wataanza ujenzi wake ambao itakuwa kilometa thelathini na moja.

Mwisho