Site icon A24TV News

Wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji yawasilisha Bajeti mwaka 2023/2024

Na Doreen Aloyce, Dodoma

Wizara ya Uwekezaji,Viwanda na Biashara imeliomba Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kupitisha bajeti la shilingi 119,017,998,000 ambazo zitaendesha matumizi mbalimbali ya Wizara hiyo.

Ombi hilo limeyolewa na Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji Dkt. Ashatu Kijaji wakati alipokuwa akiwasilisha hotuba ya bajeti Bungeni Dodoma kwa mwaka 2023/2024 ambapo amesema Kati ya fedha hizo,
shilingi75,451,494,000ni matumizi ya kawaida,shilingi 63,086,267,000 ni mishahara na shilingi 12,365,227,000 ni matumizi mengineyo.

Aidha amesema shilingi43,566,504,000zinaombwa
kwa ajili ya matumizi ya maendeleo ambapo shilingi
30,346,819,000 nifedha za ndani na shilingi 13,219,685,000ni
fedha za nje.

Vilevile amesema Katika kipindi cha Julai, 2022 hadi
Machi,2023, mambo mengi yamefanyika ikwemo Serikali kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo ilitoa
mikopo ya Shilingi bilioni 47.042 ili kuwezesha uwekezaji katika
viwanda vya uchakataji na uongezaji thamani wa mazao
mbalimbali nchini.

“Mikopo iliyotolewa imefanikisha uwekezaji katika
viwanda vipya 5 na viwanda 9 vilivyokuwepo kupitia mikopo ya
uendeshaji na ununuzi wa mashine za kisasa na Mikopo iliyotolewa kwa viwanda vipya inajumuisha kiwanda kikubwa
cha uzalishaji wa Sukari kilichopo Bagamoyo ambacho kimeanza
uzalishaji kwa kusaga tani 1,500 za miwa kwa siku “amesema Dkt Kijaji.

Pia amesema Serikali imewekeza katika kiwanda cha kukoboa mpunga na utengenezaji wa chakula cha mifugo chenye
uwezo wa kukoboa tani 192 za mpunga kwa siku pamoja na
kutengeneza tani 240 za chakula cha mifugo kwa siku.

Dkt. Kijaji amesema kuwa
Katika mwaka wa fedha 2023/2024, Wizara
imepanga kutekeleza malengo ya kuboresha Mazingira ya Biashara hapa nchini na nje ya nchi kwa Kuanzisha muundo wa ufuatiliaji na tathmini wenye ufanisi
katika kukuza biashara.

Pia amesema Kuhamasisha na kuratibu majadiliano ya kisekta
yanayopelekea maboresho ya mazingira ya biashara na
Kuhakikisha majukumu ya mamlaka za udhibiti yanayoingiliana
yanaondolewa na yanayofanana yanaunganishwa.

“Lakini pia malengo ya wizara katika kuboresha viwanda ni Kuwa na takwimu, tathmini na taarifa zitakazowezesha
kuendeleza sekta ya Viwanda,
Kuwezesha uanzishwajiwa viwanda vipya na kongani za
viwanda, Kuendelea na utekelezaji wa miradi ya kimkakati na kielelezo”

“Kufanya majadiliano na mwekezaji ili kusaini Mkataba wa ubia Pamoja na kulipa leseni za uchimbaji wa Makaa ya Mawe
Katewaka,Kufanya utafiti wa kina wa kijiolojia na Kulipia leseni za uchimbaji katika Mradi wa Makaa ya Mawe Muhukuru” amesema Dkt Kikaji.

Pia amesema serikali ina mkakati wa Kuendeleza kiwanda cha KMTC katika Mkoa wa kilimanjaro kuendelea kutafuta masoko
kwa ajili ya bidhaa zinazozalishwa hapa nchini ili wananchi waweze kufaidika.

Mwisho.