Site icon A24TV News

Update : Kuhusu Kesi ya Wanavijiji wa Loliondo dhidi ya Waziri wa Utalii na Maliasili

Na Mwandishi wa A24Tv .

Leo Tarehe 15.05.2023 saa 4Asubuhi Shauri No. 21 ya Mwaka 2022 kuhusu Maombi ya Mapitio ya Sheria (Judicial Review Application) dhidi ya Tangazo la Waziri wa Mali asili na Utalii (GN no 421 ya tarehe 17 Juni 2022 kuhusu ardhi ya Vijiji vya Loliondo kuwa Pori Tengefu la Pololeti ,linakuja kwa ajili ya Maamuzi madogo mbele ya Jaji Tiganga.

Katika shauri hilo Waleta maombi Watano kutoka vijiji vilivyoathirika wanaomba Mahakama:

1) Iagize Serikali kuondoa zuio dhidi ya Wananchi kuingia kwenye eneo la Km2 1502 ambalo wamekuwa wakitumia kwa ajii ya malisho ya mifugo yao na kwa ajili ya kufanyia shughuli za imani yao

2) Mahakama itengue Tangazo la Serikali (GN421) la tarehe 17 Juni 2022 kuwa ni batili na limetangazwa kinyume na sheria na pia haikuwashirikisha wananchi kama sheria inavyotaka

3) Mahakama itamke kuzuia Serikali na Mawakala wake wasifanye oparesheni zote kwenye eneo hilo