Site icon A24TV News

WIZARA YA ELIMU YATUMA SALAMU NZITO KWA SHULE ZINAZO KIUKA MAADILI YA NCHI ! IKIWEMO MASWALA YA USHOGA NA UKATILI

Na Geofrey Stepben 24tv Arusha .

Katibu Mkuu wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof, Carolyne Nombo ameielekeza ofisi ya mdhibiti ubora wa elimu hapa nchini kuendelea na kufuatilia shule zote za binafsi ili kuweza kubaini shule zinazo fundisha mapenzi ya jinsia moja (ushoga).

Prof, Nombo ameyasema hayo leo alipo kuwa akifungua mkutano wa 31 wa Baraza la wafanyakazi wa elimu Jijini Arusha kwa niaba ya Waziri wa elimu,Sayansi na Teknolojia Prof, Adolf Mkenda.

Katibu Mkuu wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia  akizungumza na wajumbe wa mkutano huo

Ameeleza kuwa ni vyema kwa Mkurugenzi wa udhibiti ubora kupiga hatua tatu mbele zaidi ili kuweza kukabiliana na changamoto hiyo ambayo hivi sasa inaonekana kukithiri hapa nchini hasa swala zima la unyanyasaji na ukatili wa jinsia kwa wanafunzi mashuleni.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Akiteta neno na Mkuu wa Wilaya Arusha Felishian .

“Nikuombe Mkurugenzi wa udhibiti ubora kuzidi kupambana na swala hili maana tunapambana kukuza elimu yetu niombe ofisi yako isilale izidi kupambana na mambo haya ya ushoga yanazidi kukithiri hasa shule zetu za binafsi zinanyooshewa vidole sana mzifatile na muweze kuzibanini ili tuweze kuzichukulia hatua kwa haraka”. Alisema Prof Nombo.

“Pia tuwe wakwanza kuhabarisha umma katika vitendo hivi vya unyanyasaji na mapenzi ya jinsia moja kwa watoto wetu, ulawiti pamoja na ndoa za utotoni, Sisi kama sekta ya elimu tunakutana na mambo haya mashuleni sasa naomba tuwe wa kwanza kuyasemea ili jamii ijue na kuyapinga na mwishowe watoto wapate ili bora na stahiki”. Aliongeza Prof Nombo.

Wajumbe wa Mkutano wakifatilia Mkutano kwa umakini.     Aidha Prof, Nombo amesema serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imedhamilia kuleta mageuzi makubwa kwa wanafunzi kupata elimu bora ikiwemo kujiamini, kujiajiri na kuajirika kitaifa na kimataifa, Pia amemshukuru Rais kwa kuendelea kutia fedha za miradi mbali mbali ya elimu hapa nchini.

“Serikali kupitia wizara yetu ya elimu,sayansi na teknolojia imedhamilia kuleta mageuzi makubwa kwa wanafunzi kuoata ajira na ndiyo maana Wizara imezingatia soko la ajira ya ndani na nje ili kuwedha kukidhi soko la kimataifa kwa wanafunzi wetu wanapo kuwa wakihitimu masomo yao ya elimu mbali mbali”. Amesema Prof Nombo.

Pia Prof Nombo, ameeleza kuwa ili kuweza kukuza ubora wa elimu wizara inaendelea kutoa mafunzo ya vitendo kwa walimu wa sayansi, wakufunzi wa vyuo na wataalamu mbali mbali wa elimu kwa njia ya tehama lengo likiwa ni kuwafikia kwa wigo mpana na kwa wakati.

Prof, Nombo amebainisha kuwa hadi sasa serikali imeweza kununja vifaa visaidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum waliyopo mashuleni pamoja na vyuoni kimasomo lengo likini ni ufanikishwaji wa utoaji elemu stahiki kwa wanafunzi wa aina zote pasipo kuwa ubaguzi maana wote wanaingia katika soko la ajira.

“Rai yangu kwenu niwaombe tuendelee kushikamana katika utendaji kazi wa wizara yetu kuendelea kutoa elimu bora maana wizara yetu ndiyo tegemeo zaidi katika ustawi wa elimu hapa nchini niwaombe tufanye kazi zetu kwa nidhamu kubwa na kupambana na hali iliyopo sasa katika jamii zetu”. Alisema Nombo.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe, Felishian Mtehengerwa amesema kwasasa elimu ya Tanzania inakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hajakosea kuwachagua viongozi hao kuisimamia wizara hiyo maana wanafanya kazi nzuri na kuwataka wawe wakali katika usimamizi wa shule za binafsi ambazo hadi sasa ndizo zinaongoza kwa janga la mapenzi ya jinsia moja.

Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya Felishian Akifungua Mkutano huo kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Mtahengerwa amesema kuwa kwasasa kuna wimbi kubwa la watu mashuleni kupandikiza mizizi ya mapenzi ya jinsia moja na kueleza kwamba zipo shule ambazo zimewekwa hadi nembo inayo ashiria mapenzi ya jinsia moja na kumekuwa na watu waokuja kwa nia ya utoaji elimu kumbe ndani yake wanania zao ovu.

“Kuna watu wanakuja kwaajili kutoa elimu wala uongozi haujui wanakuja na mambo yao ya ajabu na maovu kwa watoto wetu jambo ambalo tunaangaika nalo na sisi kama Arusha tayari tumeanza na kwa wale wote watakao bainika tutawachukulia hatua kali za kishelia”. Amesema Mtehengerwa.

“Pia kuna jambo ambalo bado linaukakasi katika sekta hii ya elimu ni swala zima la ulawiti na unyanyasaji wanao ufanya walimu wetu mashuleni na pindi mtoto anapo ulizwa akisema ni mwalimu ndiyo kamfanyia utaona shule husika kumfivhia siri kwa kuogopa sifa mbaya ya shule na taaluma ya mwalimu pasipo kujua yeye ndiyo amevunja sheria”. Ameongeza Mtehengera.

Aidha Dc Mtahengerwa amewataka chama cha wafanyakazi wa sekta ya elimu kufanya kazi yao ya kuwatetea watu wao na kuacha tabia ya kuwa watumwa kwa nasiasa na kuacha majukumu yao na kujisahau kama wao pia niwafanyakazi wanahitaji kujitetea kisa wamepata nafasi ya kuwaongoza wengine.

Katika hatua nyingine Mtahengerwa ameiomba wizara ya elimu kuendeleza zaidi utoaji wa elimu bora na kuzipita nchi za Afrika ya Mashariki ili kuliweka taifa kati soko lisilo shuka kimataifa kwa kuzalisha wataalam bora na wenyesifa za kimataifa.

” Kwasasa elimu yetu ni bora zaidi katika ukanda huu ya nchi za Afrika Mashariki niwapongeze kwa jinsi mnavyo pambana na mitaala ili iweze kuendana na soko la ajira la kimataifa niwaombe muongeze zaidi tuweze kuzishinda nchi zetu tunazo pakana nazo ambao wao wanaongeza kwa lugha ya kingereza kitu ambacho kinatufanya Tanzania tusionekane kama sisi ni bora kuliko wao katika utendaji kazi”. Alisema Mtehengerwa.

Idha ikubumkwe mkutano huo wa 31 wa Baraza la wafanyakazi wizara ya elimu,sayansi na Teknolojia utafanyika kwa siku mbili Jijini Arusha ambapo u aongozwa na kaulimbiu isemayo “SERA NA MITAALA BORA KWA MAENDELEO YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA BUNIFU”

Mwisho.