Site icon A24TV News

WAZIRI MCHENGERWA MIRADI WALIOPEWA WAKANDARASI SITAKI KUONA UKIRITIMBA

Na Geofrey Stephen Arusha

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa amesema kuwa hakutakuwa na muda wa nyongeza katika utekelezaji wa miradi nane ya Redgrow yenye thamani ya sh, bilioni 157.2.

Mradi huo unalengo la kutangaza vivutio vya utalii katika mikoa ya kusini utakapokamilika na umegawanyika katika makundi mawili yenye⁰01qz maeneo manne,manne ikiwemo uboreshaji wa viwanja vya ndege.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mikataba nane ya ujenzi wa majengo ya utalii,ujenzi wa viwanja vya ndege aliisisitiza hatasita kuwachukuliwa hatua wakandarasi watakaopewa kazi ya kujenga vivutio hivyo na majengo kwani mkataba huo umecheleweshwa kwa zaidi ya miaka minne.

Alisema viwanja sita vya ndege vitajegwa ikiwemo Hifadhi za Ruaha viwanja vitatu, Hifadhi ya Mwalimu Nyerere viwanja viwili na Hifadhi ya Mikumi kiwanja kimoja

Alisema katika hifadhi ya Udzungwa itajengwa njia njia ya juu ya utalii ya kilomita moja ambayo itakuwa njia ndefu katika njia zote Kusini mwa Afrika au Katika Nchi zaAfrika Mashariki.

Alisema pia vitu mbalimbali vitajengwa katika kuimarisha utalii na kutoa rai kwa wakazi wa mikoa ya kusini kuchangamkia fursa hivyo ya ujenzi wa miradi hiyo.

Alitoa rai kwa Tanapa kukuza utalii Kusini mwa Tanzania ili watanzania waone thamani ya miradi mbalimbali inayotekelezwa.

“Acheni ukiritimba lazima tubadilike miradi huu u
ulikuwa ufanyike mwaka 2019 mnapita huku mnaingia huku sasa hii si faida kwa nchi yetu, simamieni mikataba acheni ukiritimba katika utekelezaji wa miradi mbalimbali haiwezekani Rais Samia Hassan Suluhu aseme ameleta miradi Kusini halafu watu wanakwamisha hapa lazima tuhakikishe mambo yaliyokwama yanafanya kazi ndio maana tunakwamua mambo mbalimbali yaliyokwama ”

Naye Katibu Mkuu waWizara hiyo,Dk, Hassan Abbasi alisisitiza milango ya kufungua fursa za utalii Mikoa ya Kusini ifunguliwe ikiwemo kusaini mikataba hiyo nane kwaajili ya uboreshaji wa miundimbinu lengo ni kufungua fursa za utalii.

Alitoa rai kwa maofisa manunuzi watakaokwamisha ucheleweshaji wa miradi ikiwemo mikataba mirefu atasaidiwa pa kwenda na kusisitiza kuwa iwe mchana au usiku mikataba hiyo ikamilike kwa wakati.

kwa upande wao wakandarasi walio sainishwa mikataba iyo kutoka kampuni za Nanara Engineering construction Campany  ltd  Durga Prasad na mkandarasi Hainan International ltd Mr zhou Tao wamesema wataakikisha wanafanya kazi hizo kwa muda walio kubaliana na kwamba livha yakutomuwepo kwa muda wa nyongeza watamaliza kwa wakati .

Naye mkandarasi wa kampuni ya Badr East African Enterprises Ltd kupitia kwa mratibu wake Richard Magoyo wanao jenga mradi wa kiwanja cha ndege  ifadhi ya Mikumi amesema aoni changamoto yoyote itakayo wakwamisha katika utekelezaji wa mradi huo kwani mikataba imejieleza na hivyo wizara itegemee kazi nzuri itakayo malizika ndani ya muda walio pewa .

Mwisho