Site icon A24TV News

Tanzania na Malawi kukuza uhusiano wa kibiashara na uwekezaji

Na Mwandishi aa A24Tv .Malawi

Tanzania na Malawi zimekubaliana kukuza uhusiano wa kibiashara na uwekezaji kwa kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji baina ya nchi hizo ikiwemo uboreshaji wa sheria za uwekezaji, ukamilishaji wa ujenzi wa Kituo cha Pamoja cha Kasumulo na huduma za Bandari ya Mbamba Bey ili kukuza biashara na uchumi katika nchi hizo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Ashatu Kijaji akihutubia Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi linalofanyika 26 – 29/04/2023 Mzuzu Malawi.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah Aprili 26, 2023 kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Ashatu Kijaji alipokuwa akihutubia Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi linalofanyika 26 – 29/04/2023 Mzuzu Malawi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah (katikati) kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Ashatu Kijaji akiwa na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Malawi Mhe. Simplex Chithyola Banda (Mb.) (wapili kushoto) wakikagua mashine ya kukamulia maziwa kutoka Tanzania katika maonyesho ya bidhaa wakati wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi linalofanyika 26 – 29/04/2023 Mzuzu Malawi.

Aidha, amesema Tanzania inawakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Malawi kuja kuwekeza na kufanya biashara Tanzania katika sekta za kilimo, uvuvi, uchumi wa bluu, uzalishaji utalii, huduma za fedha, uchukuzi, miundombinu, mawasiliano, madini elimu na afya ili kukuza biashara na uchumi wa nchi hizo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah (kulia) kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Ashatu Kijaji akiongea na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Malawi Mhe. Simplex Chithyola Banda (Mb.) (kushoto) wakati wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi linalofanyika 26 – 29/04/2023 Mzuzu Malawi.

Vilevile amewataka wafanyabishara na wawekezaji wa Tanzania kutumia kikamilifu fursa zinazopatikana baina ya nchi hizo kulingana na raslimali zilizopo katika nchi hizo ili kuongeza kasi ya ukuaji wa biashara ambayo imefikia kiasi cha dola za Marekani milioni 86.7 mwaka 2022.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah (Kushoto) akiwa na Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi Mhe. Humprey Polepole (wapili kushoto) wakishiriki
Konamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi linalofanyika 26 – 29/04/2023 Mzuzu Malawi.

Naye Waziri wa Biashara na Viwanda wa Malawi Mhe. Simplex Chithyola Banda (Mb.) amesema Malawi iko tayari kuimarisha uhusiano wa kibiashara na uwekezaji baina ya nchi hizo uliopo tangu Uongozi wa Serikali ya Awamu ya kwanza ya Tanzania kwa kuendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini humo.

Waziri wa Biashara na Viwanda wa Malawi Mhe. Simplex Chithyola Banda (Mb.) (kulia) akifungua Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi linalofanyika 26 – 29/04/2023 Mzuzu Malawi.

Aidha amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Smia Suluhu Hassan kwa Msaada wa chakula na vifaa vya kujihifadhi alioutoa wakati Malawi ilipokumbwa na kimbunga freddy Machi 2023

Wafanyabiashara wa Tanzania wakishiriki Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi linalofanyika 26 – 29/04/2023 Mzuzu Malawi

Kwa upande wa Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi Mhe. Humprey Polepole amesema kongamano hilo limewakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji zaidi ya 300 kujadili, na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili katika biashara zao baina ya nchi hizo. Pia amewashauri watanzania kuwa wabunifu na kushirikiana na wafanyabiashara wa Malawi kutumia fursa za biashara na uwekezaji zilizopo nchini Malawi ambayo ni moja ya nchi sisizokuwa na bahari

Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi Mhe. Humprey Polepole ( kushoto) akiongea na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Malawi Mhe. Simplex Chithyola Banda (Mb.) (kulia) wakati wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi linalofanyika 26 – 29/04/2023 Mzuzu Malawi.

Picha ya pamoja ya viomgozi wa Tanzania na Malawi walioshiriki Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi linalofanyika 26 – 29/04/2023 Mzuzu Malawi

Mwisho