Site icon A24TV News

SERIKALI KUENDELEA KUJENGA MAGALA KUDHIBITI SUMU KUVU

Na Geofrey Stehen Arusha

Serikali imeendele kujenga maghala ya kuhifadhia mazao Nchini Ili kuzuia sumu kuvu Hali inayochangia Athari kwa wazalishaji na wakulima

Katibu mkuu wizara ya kilimo Gerald Mweli akifungua kikao Cha washiriki wa sekta ya kilimo jijini Arusha kilichohusisha nchi 11, alieleza nilazima kuwepo kwa mifumo thabiti itakayosimamia masuala mazima ya kilimo na utoshelezi wa chakula.

Ameseema Tanzania imepata dola za kimarekani milioni 20 zilitolewa kama msaada wa mapambano ya sumu kuvu Licha ya kuonekana Athari za Awali ,kupitia fedha hizo tayari serikali imekwishajenga maghala na maabara katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya manyara,morogoro,Dodoma, ambayo wakulima walikumbana na changamoto .

Alisema walianza kujenga Maghala hayo katika mikoa ya Manyara, Morogoro na Dodoma kutokana na tatizo hilo kuonekana kuwa kubwa katika mikoa hiyo ambapo pia alisema walishajenga Maghala 10 katika mikoa Mbalimbali ya Tanzania na maabara mbili za kupima sumu kuvu.

Aliongeza kuwa baada ya mkutano huo washiriki watapaswa kukaa pamoja kuweka mikakati mizuri ya kufanya katika kusaidia wakulima namna Bora ya kuhifadhi mazao na kuondokana na tatizo hilo la Sumu kuvu katika nchi hizo.

“Tumekubaliana kuwa baada ya mkutano huu washiriki ambao miradi hii inatekelezwa katika nchi zao waweke mfumo mzuri wa kuwaelimisha wakulima na wazalishaji wa Chakula juu ya Uwepo wa sumu kuvu lakini pia ifike mahali tusiagize Tena vyakula nje tuweze kuwa na Uzalishaji unaotosheleza”Alisema Mweri.

Naye Mwakilishi kutoka Benki ya maendeleo ya Afrika Philip Boahen alisema kutokana na Uzalishaji wa chakula kushuka barani Afrika kutokana na Kipindi Cha COVID 19 waliamua kutoa mkopo huo Ili kuinusuru Hali ya chakula hivyo alisema lengo ni kuinua Uzalishaji Kwa kasi.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

“Tunajua namna gani Uzalishaji wa chakula ulishuka kutokana na janga la Corona hivyo tumeona ni vema kuliangalia suala la Uzalishaji wa chakula na kuwekeza katika miradi hii ambapo tunanchi 13 zinazotekeleza programu hii” alisema Boahen.

Halikadhalika mkutano huo unadumu Kwa siku nne mkoani Arusha na nchi 11 zimeweza kutuma washiriki katika mkutano huo huku mkutano huo ukiratibiwa na Benk ya maendeleo ya Afrika

End

Mwishooooo.