Site icon A24TV News

NI HISTORIA KUMBUKIZI YA KUZALIWA NABII MKUU DK GEORDAVIE MAELFU WAMPONGEZA WAPO VIONGOZI WA SERIKALI KUTOKA NDANI NA NJE YA NCHI

Kuhusu siku yake ya kuzaliwa Nabii Mkuu Mh  GeorDavie kwanini kuna kuwa na kumbikizi ? 

Na Geofrey Stephen Arusha .

Tarehe 25 Mwezi April ni kumbukizi ya Nabii Mkuu Mh Dokta  GeorDavie kukumbuka siku yake ya kuzaliwa ambapo Maelfu ya  waumini wa huduma ya Ngurumo ya Upako walisherekea kwa pamoja huku wageni kutoka nchi mbali mbali   kutoka nchini  Congo, South Africa, Kenya na maeneo mbali mbali ya pembezoni  ya dunia  walikuwepo katika siku hii muhimu kwa Nabii Mkuu.

Awali akizungumzia siku hiyo muhimu kwake Mh Nabii Geordavie Mkuu amesema kwamba siku hiyo ilikuwa ifanyike tarehe 25 mwezi April lakini kutokana na siku hiyo kuangukia siku ya kazi na sio siku ya huduma, hivyo kupelekea kufanyika siku ya juma pili ya tarehe 23 kwa lengo  la wana Ngurumo kupata fursa ya kusherekea pamoja na Nabii Mkuu Mh Dokta  GeorDavie .

Nabii mkuu akizungumza katika ibada ya kumbukizi yake ya kuzaliwa amesema kuwa wanadamu wanapaswa kujifunza kupambanua nyakati katika maisha kwani kila jambo lina majira yake ikiwemo nyakati za kufurahia ,kulia na kutafakari maisha.
Nabii Mkuu Mh Dokta GeorDavie amesema wakati anakumbuka siku yake ya kuzaliwa anashukuru Mungu amefanikiwa kusaidia jamii katika kutoa misaada mbali mbali ikiwemo mitaji kwa vijana wanawake wazee na rika mbali mbali ambapo mpaka kufikia mwaka huu wa 2023 amesha tumia kiasi cha shilingi Milioni 400 kugusa jamii katika kutoa mitaji kugawa piki piki bajaji vifaa vya studio kwa wasanii , mitaji kwa wafanya biashara  wa soko la Samunge jijini Arusha na wengine wengi kutoka mikoani pamoja na nje ya nchi ambapo Nabii Mkuu Mh Dokta GeorDavie amegusa jamii kwa mahitaji muhimu .
Amesema kuwa, unapo ongeza siku katika maisha unatafakari ulipo toka ulipo na unapo kwenda katika maisha huku nafasi kubwa ukisaidia jamii kwani utajiri Mungu aliokupa unatakiwa kugusa jamii kwani utajiri mwingi una makusudi yake na mimi mwenyewe Mungu ameniinua kwa lengo la kugusa jamii kwani najua maisha niliyo toka .
Nabii Mkuu amesema unapoongeza siku majukumu yako yanazidi kuongezeka hivyo ni vizuri kutumia vyema nafasi yako usije kujutia kwanini ulibweteka kufanya mambo muhimu katika maisha yakiwemo maendeleo kuombea nchi ,Viongozi wakuu wa Serikali pamoja na kuombea jamii ndogo yenye uhitaji kila siku
Baadhi ya wasanii waliohudhuria sherehe hiyo ya kihistoria ya Nabii Mkuu Mh GeorDavie  ,Msanii Kidumu kutoka nchini kongo 20pecent kutoka Tanzania ambao walishikwa mkono na Nabii Mkuu na walitabiriwa kufika mbali pamoja na wasanii wengine wengi kutoka Congo, Kenya na hapa Tanzania katika mikoa ya Dar es Salaam   , Dodoma na  Arusha .
Mwisho .