Site icon A24TV News

JK White Cement (Africa) Ltd yawanoa mafundi rangi zaidi ya 200 Arusha

Na Mwandishi A24tv .Arusha,

Kampuni ya JK White Cement (Africa) Ltd kupitia bidhaa yake ya JK Wall Putty imefanikiwa kuwakutanisha zaidi ya mafundi rangi 200 wa jijini Arusha kwa ajili ya kuwapa elimu na kujadili changamoto wanazokumbana katika kazi zao za skimming.

Akizungumza kwenye semina hiyo ya siku moja, Afisa kitengo cha ufundi kwa wateja Simioni Ogudumu alisema kuwa wameamua kukutana na mafundi hao kwa ajili ya kuwaelekeza kuhusu bidhaa zao lakini pia kujadili changamoto wanazokumbana nazo kazini.

“Tumekuwa tukipokea sim nyingi za wateja wetu ambao ni mafundi juu ya changamoto za uelewa wa jinsi ya kutumia bidhaa zetu hivyo tumekuja kuwaongezea uelewa kwa ajili ya kupata matokeo mazuri zaidi”

Mmoja wa mafundi wahudhuriaji katika semina hiyo, Glory Msuya mtaalamu wa kupaka rangi nyumba alisema kuwa wamekuwa na changamoto nyingi wanazokumbana nazo kwenye kazi katika matumizi ya bidhaa mbali mbali za umaliziaji wa nyumba

“Matokeo ya bidhaa za JK Wall Putty ni mazuri kutokana na hali ya hewa ya Arusha hasa kipindi cha mvua lakini pia aina ya udongo na miundo mbinu zingine tofauti na bidhaa zingine huko nyuma ambazo zimekuwa na changamoto kubwa za utumiaji”

Nae Abdi Masita alisema kuwa Arusha kuna changamoto kubwa ya magadi na fangas hivyo matumizi ya bidhaa sahihi kwa mchanganyiko wa bidhaa za JK White Cement (Africa) Ltd zimekuwa mkombozi kwao

Kwa upande wake afisa masoko wa kampuni ya JK White Cement (Africa) Ltd Ms Merbo Haule aliwataka mafundi hao ili waweze kunufaika na kazi zao lazima watumie bidhaa sahihi na zenye ubora na wawe wanajitangaza ili pia wapate kazi za taasisi na makampuni makubwa.

“Unakuta mafundi wanafanya kazi zao nzuri lakini lakini wanatumia bidhaa zisizo na ubora na kufanya kimya kimya bila hata kupiga picha wala kujitangaza ndio maana kazi kubwa zinawapita na kubaki na kazi ndogo ndogo mtabaki hivyo hivyo badilikeni ili mnufaike na kazi zenu”

Mwisho…