Site icon A24TV News

SERIKALI YAFUNGIA MGODI WA GEM AND ROCK VENTURE ULIOKO MIRERANI

Na Mwandishi wet Arusha

Mgodi wa Madini ya Tanzanite wa Gem & Rock Venture Uliopo Kitalu B Mirerani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara umefungwa kuendesha shughuli za uchimbaji na Wizara ya Madini baada kukaidi Mara mbili kuamuriwa kusitisha shughuli za uchimba pale ulipolalamikiwa na Kampuni ya Franone inayochimba Mgodi wa Kitalu C kwa kushirikiana na serikali Kama mbia Mwenza.

Mbali ya Hilo Watalaamu wa Chuo Cha Madini Mkoani Dodoma wanaotarajiwa kuwasili leo Jijini Arusha kupima Madini yaliyokamatwa katika vurugu hizo Kama ni Mali ya Kitalu B au C na hiyo ndio itaondoa utata kwa pande zote juu ya kukamatwa kwa Madini hayo.

Akizungumza na Gazeti hili kwa Njia ya simu ya kiganjani Afisa Madini Mfawidhi Mkoa  Mkoa wa Manyara,Mernad Msengi alisema jukumu la wataalamu hao kuangalia Kama Madini yaliyohifadhiwa na ofisi yake Kama kweli yanatoka Kitalu B au C kufanya hivyo kwa Wizara ya Madini ni ukaidi wa viongozi wa Gem & Rock Venture.

Msengi alisema kuwa Wataalamu hao Ndio Wenye kumaliza mgogoro na utata wa Madini hayo yenye uzito wa kilo kadhaa Kama kweli Madini hayo yamechimbwa katika Mgodi B au C na amewataka viongozi wa Mgodi wa Gem & Rock Venture kuacha kutafuta huruma kwa jamii kwani timu itakayokuja itasema ukweli na hakutakuwa na longolongo.

Akizungumzia madai ya wafanyakazi wa Gem & Rocky Venture kupigwa na Polisi,Maofisa Usalama wa Taifa ,Maofisa wa Wizara ya Madini na JWTZ,Msengi alisema madai hayo Yana lengo potofu na amewataka viongozi wa Mgodi wa Geme & Rock Venture unaomilikiwa na Sammy Mollel na Joel Mollel Maarufu kwa jina la Saitoti kuacha propoganda na kuviachia vyombo vya Dola kufanya kazi yake bila kuingiliwa mtu yoyote.

Msengi alisema sakata la  vurugu zilizoibuka ndani ya Mgodi wa Tanzanite wa Kitalu C unaomilikiwa na kampuni ya Franone chini ya Ukurugenzi wa Onesmo Mbise Maarufu kwa jina la Onee na Mgodi wa Kitalu B unaomilikiwa na kampuni ya Gem & Rock Venture chini ya wakurugenzi Mollel na Saitoti kuwaagiza wafanyakazi wao kukaa kimya kwani kwa Sasa sakata hilo liko katika mikono ya Wataalamu na Dola.

Hivi karibuni ilidaiwa kuwa wafanyakazi 30 wa Kampuni ya Gem & Rock Venture walivamia mgodi wa Kitalu C na kuchimba Madini ya Tanzanite kibabe ndani ya mgodi huo na kufanikiwa kupora Madini hayo lakini uongozi wa Kampuni hiyo ulipinga na kusema kuwa wao ndio wameporwa Madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 6 yenye thamani ya Mamilioni ya pesa na Maofisa wa Wizara ya Madini kwani walikuwa wakizalisha kwa siku tatu mfululizo kabla ya kuporwa ndani ya mgodi wao wakati Madini hayo yakiwa na Seal ya Wizara.
Mwisho