Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Mahakamani»MFANYA BIASHARA WA MADINI YA TANZANITE SAITOTI NA WENZAKE WAFIKISHWA MAHAKAMANI WASOMEWA MASHTAKA YANAYO WAKABILI

    MFANYA BIASHARA WA MADINI YA TANZANITE SAITOTI NA WENZAKE WAFIKISHWA MAHAKAMANI WASOMEWA MASHTAKA YANAYO WAKABILI

    0
    By arushatv on March 17, 2023 Mahakamani

    Na Mwandishi wetu ,Simanjiro

    Mfanyabiashara Maarufu wa Madini ya Tanzanite Jiji la Arusha Joel Mollel Maarufu kwa jina la Saitoti ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Gem & Rock Venture na wenzake saba  wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kujibu Mashtaka mawili ya shambulio na kukaidi amri ya Wizara ya Madini katika tukio lililotokea march 13 mwaka huu katika Mgodi wa Kitalu C inayomilikiwa na serikali na Mwekezaji Mzawa Onesmo Mbise.

    Wakisomewa Mashitaka na Mwendesha Mashitka wa Polisi, Mosses Hamilton Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro, Charles Uiso ilidaiwa kuwa katika shitaka la Kwanza linalowahusu washitakiwa wote saba ilidaiwa kuwa wote kwa pamoja waliwashambulia kwa majabali na silaha za uchimbaji wafanyakazi sita wa Kampuni Franone inayochimba Mgodi wa madini ya Tanzanite kitalu C kwa kushirikiana na serikali.

    Mbali ya Saitoti walioshitakiwa wengine ni pamoja na Petro Exsaud(48) mkazi wa Moshono Arusha,Mosses Kelerwa(45) mkazi wa Mirerani,Daniel Siyaya(44) mkazi wa Ilboru Arusha, Mosses sirikwa (46) mkazi wa Ilboru,Dausen Mollel(58) Mkazi wa Ilboru na,Enock Nanyaro(32) mkazi wa Arusha.

    Katika shitaka la kwanza,Mwendesha Mashitaka wa Polisi alidai kuwa shitaka hilo linawahusu washitakiwa wote kwani ilidaiwa kuwa March 13 mwaka huu waliwashambulia  kwa majabali na vifaa bya uchimbaji wafanyakazi sita wa Franone akiwemo Benson Banash,Vedastus Swea,Alvin Msuya,Swetbert Albogast,Mussa Unambe na Bonfance Mollel

     

    Hamilton alidai kuwa washitakiwa hao walitenda kosa Hilo wakati wakijua wazi kuwa kufanya kosa hilo nikosa kisheria lakini washitakiwa wote walikana shitakana hilo na walikidhi vigezo vya dhamana kwani kila mshitakiwa alidhaminiwa na mdhamini mmoja na bBondi ya shilingi milioni moja na washitakiwa walikidhi vigezo vya dhamana na upelelezi wa Kesi hiyo bado haujakamilika kesi hiyo itatajwa tena aprill 14 mwaka huu katika mahakama hiyo.

    Kwa mujibu wa Mwendesha Mashitaka wa Polisi alisoma shitaka la pili linalowahusu washitakiwa wawili akiwemo

    Saitoti na Joel Mollel (50) ambao ilidaiwa wameshitakiwa kwa kwa shitaka moja la kukaidi amri ya Wizara ya Madini ya ambapo ilidaiwa kuwa walizuiwa kufanya shughuli za uchimbaji baada ya mtobozano na Kitalu C lakini walikaidi na kuendelea na kazi wakati wakijua wazi ni kosa.

    Washitakiwa walikana shitaka hilo na walipewa dhamana ya mtu mmoja mmoja na kufanikiwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuweka Bondi ya shilingi milioni moja na kwa mujibu wa Mwendesha Mashitaka wa Polisi alidai kuwa upelelezi wa Kesi hiyo umekamilika na washitakiwa wataanza kusomewa Maelezo ya Awali April 14 mwaka huu.

    Mwisho

    Post Views: 33
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticlePANGA LASAMIA LAPITIA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA ! MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA24TV
    Next Article MAJALIWA AWASHIA MOTO WAKUU WA WILAYA ! MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA 24TV

    Related Posts

    Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imetoa amri ya kufika mahakamani kwa wajibu maombi kwenye kesi ya kulazimishwa kupotea

    March 23, 2023

    RUFAA YA WANANCHI WA LOLIONDO YASIKILIZWA NA JOPO ZITO LA MAJAJI WATANO

    February 7, 2023

    JELA MIAKA MINNE KWA KUMKATA BOSI WAKE KIGANJA CHAMKONO

    January 24, 2023

    JELA KWA KOSA LA KUMLAWITI KIJANA WA MIAKA15

    January 17, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.