Site icon A24TV News

MBUNGE WA EALA JAMES OLE MILYA AJITOSA KUGOMBEA NAFASI YA MNEC ANAHISTORIA KUBWA NA CHAMA

Na Geofrey Stephen Arusha .

Vigogo wamejitokeza kuwania nafasi za wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Arusha.

Miongoni mwa waliojitokeza kuwania nafasi hizo ni Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki(EALA) James ole Millya na wengine wanne ambao wamekwenda Ofisi ya  katibu wa CCM Mkoa Arusha  kimya kimya kukabidhiwa fomu na sekretari wa chama ambaye hakupenda kutaja jina lake baada ya Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha,Mussa Matoroka kuwa kwenye ziara ya Utelelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoani.

Mbunge wa EALA James Ole Milya amizungumza na vyombo vya habari kuhusu Kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Mnec

Alisema yeye ni mbunge wa EALA lakini ameona ni vema agombee nafasi hiyo ili kuusaidia Mkoa wa Arusha ambao ni lazima timu imara iwepo kuhakikisha chaguzi zijazo chama kinashinda kwa kishindo .

Alisema yeye kama kijana aliyepikwa na chama amejitoa kuwania nafasi hiyo ili kusaidia chama kushinda kwani  anajua vema siasa za nchi ya Tanzania na kingine asingependa kusikia jimbo la Arusha ni la upinzani bali jimbo ni mali ya Ccm kama ilivyo sasa .

Alimpongeza Rais Samia Hassan Suluhu kwakuruhusu mikutano ya Vyama vya Siasa hivyo kutokana nauzoefu wake katika nafasi zake alizokuwa nazo awali anaamini akipata nafasi ya ujumbe wa Halmshauri kuu .

Mbunge James Ole Milya akionyesha fomu kwa vyombo vya habari mara baada ya kuchukua .

“Ninauzoefu wa kisiasa na naomba ridhaa ya kuwania nafasi hii kwani sifa na uzoefu wa pande zote mbili katika chama ninao”

Milya  ni Miongoni mwa vijana machachari wenye historia kubwa sana katika uwongozi na anapo jaribu nafasi ya kugombea ushawishi wake ni mkubwa sana .