Site icon A24TV News

JIJI LA ARUSHA LATOA MIKOPO YA SHILINGI BILION 2.6 KWA VIJANA WENYE MAITAJI MAALUM NA WANAWEKE

Na Geofrey Ste,Arusha

Jiji la Arusha limetoa mikopo ya asilimia kumi ya sh,bilioni 2.656 Kwa vikundi 169 kwaajili ya makundi ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu

Aidha Watu wenye ulemavu wanaruhusiwa kukopa mikopo hiyo bila kuwa na kikundi na dirisha lipo wazi na kusisitiza Jiji litaendelea kutoa mikopo kwa njia ya mtandao ili kupata takwimu sahihi za wanufaika.

Akishuhudia zoezi la utoaji mikopo hiyo ya asilimia 10 kwa wanawake,vijana na watu wenye ulemavu,Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtahengerwa amesisitiza wanaopewa mikopo kuwa wafanyabiashara wenye ubunifu na kuacha biashara za mazoea.

Dc Mtahengerwa alisisitiza endapo wapewaji mikopo hiyo wakiwa wabunifu wataongeza tija katika biashara zao ikiwemo kufungua fursa za kutangazabiashara zao ili kupata soko la ndani na hata nje ya mkoa wa Arusha.

Alisisitiza endapo mikopo hiyo iliyotolewa na Jiji itafanyiwa kazi itapelekea kujikwamua kiuchumi na kutoa hadhari kwa wapewa mikopo kutojionyesha kuwa wanahela bali wafanye kazi

“Kinababa wake zenu wakipata mikopo msiwazuie kufanya biashara zao wala kuwaibia badala yake waacheni wabuni biashara zao ili wajikwamue kiuchumi kwani wanawake wa Arusha na makundi maalum ni wachakarikaji katika kujikwamua kiuchumi”

Pia alisema uombaji mikopo kwa njia ya kieletroniki (mtandao ) ni mzuri kwani unaonyesha vikundi vingapi vimepata mikopo na vipo wapi hivyo Jiji litaendelea kutoa mikopo kwanjia hiyo ili kujua makundi yaliyofikiwa katika utoaji na ujeshwaji wa mikopo na alimshukuru Rais Samia Hassan Suluhu kwa kuwakwamua wananchi katika hali ya chini na kufungua fursa za kibiashara.

Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha,Hargeney Chitukuro alisema mikopo hiyo haijapata kutokea mikopo hiyo itaenda kwa vikundi saba viwanda vidogo,28 wasafirishaji,77 wakulima na wafugaji na vikundi 169 vya kada mbalimbali ikiwemo wanawake,walemavu na vijana.

Alisema tangu mwaka jana hadi sasa Jiji limetoa mikopo ya sh, bilioni 3,934,133,800 ambapo vikundi vilivyofikiwa hadi sasa kwa utoaji wa mikopo kwenye vikundi 339 vikivyozalisha ajira zaidi ya 1,965.

Huku Meya wa Jiji hilo, Maximilian Irrange aliwaasa wanaochukua mikopo hiyo iwe yenye tija na kupelekea watu wengine wakope ikiwemo urekeshwaji mzuri wa marejesho.

“Msioe kwa hela za mikopo Jiji limejitahidi na Kaimu Mkurugenzi Chitukuro unajitahidi sana sana katika kuhakikisha mikopo inatoka kwa wakati lakini nyie mnaopewa mikopo hakikisheni mnarejesha kwa wakati.

Moja wa wanufaika na mkopo huo Neema Voya kutoka kikundi cha jeneevaglory kata ya kaloleni amesema watatumia vyema mikopo iyo huku akiwataka vijana wenzake kufanya kazi kwa bidii na kurudisha mikopo iyo kwa wakati kwa lengo la kusaidia wengine .