Site icon A24TV News

Wizara ya Madini imefanikiwa kutaifisha madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 4 yenye thamani ya mamilioni ya fedha  kutoka kwa Meneja wa Mgodi wa Gem & Rock Venture

Na Mwandishi wa A24Tv .

Wizara ya Madini imefanikiwa kutaifisha madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 4 yenye thamani ya mamilioni ya fedha  kutoka kwa Meneja wa Mgodi wa Gem & Rock Venture,Joel Mollel Maarufu kwa jina la Saitoti aliyevamia na kuchimba katika mgodi wa kitalu C unaomilikiwa na serikali na mwekezaji mzawa Onesmo Mbise.

Hayo yalisemwa na Afisa Mfawidhi Wizara ya Madini Mkoa wa Manyara,Mernad Msengi na kusemsa kuwa thamani halisi bado haijajulikana ya madini hayo ya Tanzanite yaliyochimbwa kwa njia haramu na Saitoti akiwa na wafanyakazi wake walioingia kitalu C marchi 12 mwaka huu majira ya saa 6.30 mchana.

Msengi alisema wa Gem & Rock Venture ambao upo katika kitalu B unamilikiwa na Mfanyabiashara Maarufu Jijini Arusha Sammy Mollel uliwahi kusimamishwa katika kipindi cha nyuma kwa kuchimba kwa njia ya wizi maarufu kwa jina la Bomu katika Kitalu C lakini wamilikiwa wa Mgodi huo wamekuwa wakaidi pindi wanapoandikiwa barua na Wizara ya Madini kusitisha uchimbaji kwa makosa hayo.

Alisema March 12 mwaka huu wamerudia kosa hilo hilo la kuingia katika mgodi huo na kuchimba kibavu na kufanikiwa kupora madini hayo yenye uzito wa kilo 4 yenye thamani ya mamilioni ya fedha na kupiga wafanyakazi ambao hali zao ni mahututi na wako hospital.

Afisa huyo wa Wizara ya Madini alisema mbali ya kutaifisha Madini hayo ya Tanzanite na kumkamata meneja Saitoti na wafanyakazi wa Gem & Rock Venture 21 pia wameufungia mgodi kwa muda usiojulikana.

Msengi hatua ambayo Wizara ya Madini imechukua kwa sasa kabla ya hatua zingine ni kuufungia Mgodi huo kuendelea kufanya kazi ili taratibu zingine za kiukaguzi ziweze kufanyika na dhidi ya wamiliki wa Mgodi huo.

‘’kwa sasa tumechukua hatua mbili,moja kutaifisha madini ya Tanzanite yaliyoporwa na Saitoti na Genge lake katika kitalu C na hatua ya pili iliyochukuliwa na Wizara ni kuufungia mgodi ili kupisha uchunguzi’’alisema Msengi

Naye Meneja wa Mgodi wa Franone unaochimba Kitalu C,Vitus Ndakize alisema kuwa siku ya uvamizi uliofanywa na Saitoti na wafanyakazi wake walipigwa wafanmyakazi wa kampuni ya Franone,askari polisi,maofisa usalama na watumishi wa Wizara waliokwenda chini ya mgodi kutekeleza majukumu ya kuwazuia kutoendelea kufanya kazi katika mgodi huo.

Vitus alisema kuwa mgodi wa kitalu C alikuwa umesimama kwa zaidi ya miaka mitano na wachimbaji haramu hao walikuwa wameingia ndani ya mgodi wa kitalu C kwa zaidi ya mita 558 katikati ya mgodi huo wa serikali na mwekezaji mzawa ,Wizara iliamua kuisimamisha Kampuni ya Gem & Rock Venture kuacha kuendelea kazi hadi hapo shauri litakapopata ufumbuzi.

Alisema wakati kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Simanjiro iliposhuka Mgodini kuangalia vurugu hizo nayo kamati hiyo ilitekwa na kupigwa na wafanyakazi hao na kujeruhiwa vibaya sana kichwani na wako na hali mbaya sana kwa sasa.

Meneja alisema kuwa wafanyakazi wa Gem & Rock Venture wamekuwa wakikaidi mara kwa mara maagizo ya Wizara pamoja na kuandikiwa barua na Wizara mara kwa mara na wamekuwa wakizalisha mara kwa mara bila Wizara kuwepo na wamekuwa wakipata madini mengi ya Tanzanite bila serikali kujua kitu ambacho serikali inakosa.

Mwisho