Site icon A24TV News

Wadau wa Tehama mkoani Arusha watakiwa kutoa ushirikiano kuhakikisha uwepo wa kituo cha ubunifu wa Tehama.

Na Geofrey Stephen Arusha

Wadau wa Tehama mkoani Arusha wametakiwa kutoa ushirikiano wa kutosha ili.kufanikisha uwepo wa kituo cha ubunifu wa Tehama kinachotarajiwa kuanzishwa  mkoani Arusha hivi karibuni.

Akizungumza katika ufunguzi huo leo jijini Arusha Kaimu Katibu Tawala msaidizi Daniel Loiruck amesema kuwa uwepo wa kituo hicho utaongeza chachu kubwa kwa vijana katika kuendeleza bunifu zao kupitia Tehama na kujulikana kimataifa zaidi.

Amesema kuwa ,uwepo wa vituo hivyo utasaidia sana kuibua vituo vya ubunifu kwa vijana kutoka katika halmashauri Ili kufungua fursa zakiuchumi kupitia Tehama.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Tehama Dr Nkundwe mwasaga amesema kutokana na uchumi wa kidigitali kukua Afrika ,wameanza na mikoa 5 ilikuifanya Tanzania kua na vijana shindani katika kuyafikia masoko makubwa nakutumia bunifu zao kukuza uchumi .

Nao baadhi ya wabuni wameomba ujezi wa vituo kiharakishwe kwa kanda ya kaskazini Ili vijana kupata ujuzi na kukuza bunifu zao.

Mwishoo