Site icon A24TV News

MZEE MOLLEL AZIKWA KIJIJINI KWAKE WANANCHI WAMWAGA MACHOZI WAZMIA WAKIAGA MWILI WAKE

 

Na Geofrey stephen Arusha .

Familia ya kijana Saitoti wakiwa katika majonzi wakiomboleza msiba mkubwa wa baba yao mzazi

Mwili wa Emmanuel Mollel ambaye ni baba wa mfanyabiashara maarufu Mkoani Arusha na Manyara umezikwa kwenyw kijiji cha Marurani wilayani Arumeru Mkoani Arusha huku maelfu ya watu wakijitokeza.

Mfanya biashara maarufu wa madini mkoani Arusha na Manyara akiaga mwili wa baba yake kwa uzuni

Joel Saitoti ni mfanyabiashara maarufu wa madini Mkoani Arusha na Manyara na mmiliki wa kampuni za uchimbaji wa madini ya Tanzanite Azo Africa Limited na Germ and Rock Ventures

Viongozi mbalimbali wakiwemo wa serikali,wananchi wachimbaji wa madini zaidi ya elfu tatu walishiriki kwenye mazishi hayo kutokana na umaarufu wa mfanyabiashata huyo pamoja na baba yake

Viongozi wa serikali na chama waliofika msibani hapo wamesema kwamba jamii imepoteza mtu muhimu sana kwani alikua na mchango mkubwa sana  kwa jamii ya kifugaji hususani vijana wanao kua walipata elimu kutoka kwake .

Msafara wa magari ya kifahari ukiwa katika msafara kuelekea nyumbani kwa mzee mollel 

Mzee Mollel amezaliwa mwaka 1945 na kufariki dunia mwaka 2023 huku akiwa na mchango mkubwa sana kwa jamii yq wafugaji na mtu mwenye wivu wa maendeleo kwa wenzake .