Site icon A24TV News

Waziri wa maliasili na utalii aitaka bodi mpya  ya Tawiri kwenda kidigitali zaidi.

Na Geofrey Stephen .Arusha.

Arusha.Waziri wa Mali asili na Utalii Pindi Chana ameitaka bodi mpya ya Taasisi ya utafiti wa wanyama pori Tanzania Tawiri kuongoza mamlaka hiyo kidigitali na kuongeza idadi ya watalii nchini kwa kufikia million  5  ifikapo  mwaka 2025.

Ameyasema hayo  leo jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya 6 ya  Mamlaka ya usimamizi na utafiti  wa wanyama pori Tanzania ( TAWIRI) ambapo amewataka  kushirikiana na mamlaka ya wanyama pori kuendeleza sekta ya utalii .

Amesema kuwa, endapo wataongeza watalii watainua mapato ya sekta ya utalii kwani  kwa sasa mapato ya mchango wa utalii kwa serikali  ni asilimia 17 hivyo kuna umuhimu wa kuongeza pato katika sekta ya utalii na Tawiri kupitia bodi yake itashauri namna ya kufikia malengo hayo.

Waziri amesema kuwa, bodi hiyo ifike wizarani kueleza changamoto ambazo zitawafanya wasifikie malengo yao katika swala zima la utafiti wa wanyama pori kwani wizara iko tayari kutatua changamoto hizo na kufikia malengo ya kuboresha tafauti za wanyama pori nchini.

“Nichukue fursa hii kuwapongeza Tawiri kwa kazi nzuri wanayoifanya katika tafiti za wanyama pori kwani tunaona kazi kubwa mnayo fanya yenye matokeo makubwa ya kubadilisha mamlaka hii ya utafiti wa wanyama pori ambapo kwa ushirikiano mkubwa kutoka kwa Mh Rais wetu Mpendwa anafuraishwa na kazi ya Tawiri ” amesema waziri.

Aidha ameitaka bodi  hiyo kufanya kazi kidigitali kwani tafiti nyingi za sasa zinafanyika kwa njia ya  digitali hivyo basi katika utumishi waweze kufanya kazi hizo kwa urahisi kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya digitali kuendana na wakati katika utafiti wa wanyama pori.

Amefafanua kuwa, wizara itaendelea kuweka mikakati ya kuboresha majengo ya utafiti katika mkoa wa Arusha na nje ya Arusha kwani kumekuwa na ukuaji wa kasi sana katika tafiti za sekta ya wanyama pori.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Tawiri David Mayanza amesema wanashukuru kwa kuweza kuteuliwa yeye na wajumbe wenzake wapatao tisa  kuunda bodi hiyo ambayo itasaidia sekta ya utalii kwani kabla ya hapo alikuwa ni makamu mwenyekiti wa bodi hiyo .

Amesema  kuwa ,watafanya kazi kwa bidii kubwa kwani bodi hiyo imepata wataalamu wenye uzoefu ambao watasaidia kuendeleza mawazo katika Taasisi ya utafiti wa wanyama pori nchini .

Aidha  ameahidi kufanya kazi za utafiti za wanyama pori kidigitali kama wizara ilivyo agiza hivyo wategemee mabadiliko makubwa sekta ya utalii na kulenga kutatua changamoto za kitafiti na kupatia majibu ya kina .

” bodi majukumu yake kuu ni kuifanya taasisi inayo iyongoza kujiendesha na kufikia mafanikio makubwa ya kujisimamia pekee yake kufikia malengo ya Tawiri katika kufanya majukumu ya kisayansi kwenda na na mabadiliko ya Teknolojia ya kitafiti .”amesema .

Amesema kuwa,  watafuata sheria na kufanya kazi kwa mpango mikakati katika kujibu matatizo ya wateja ambao ndio walengwa wakuu katika sekta muhimu ya utalii nchini.

Mwisho