Site icon A24TV News

WAFANYA BIASHARA WATAKIWA KUTUMIA FURSA KWA NCHI NANE ZA MAJARIBIO NCHINI YA MKATABA UHURU

Wafanyabiashara wameshauriwa kuhakikisha wanatumia fursa ya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi nane za majaribio za kuuza bidhaa chini ya Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) kuanzia Julai 1, 2023 kwa kupeleka bidhaa zenye viwango na ubora wa kimataifa.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) wakati wa Mkutano wa kuwajengea uwezo na kuwahamasisha Wanyabiashara kuhusu kuchangamkia fursa za biashara chini ya AfCFTA uliofanyika Januari 24,2023, JNICC Dar es Salaam.

Aidha, Dkt Kijaji amesema kuwa malighafi zikipelekwa nje ya nchi zinawanyima watanzania ajira na zinapoxhakatwa na kuletwa nchini tunazinunua kwa gharama kubwaa. Hivyo ni bora kutumia soko la AfCFTA ambalo masharti yamepunguzwa na unaweza kuuza bidhaa katika nchi 54 bila ushuru.

“Wanawake na vijana mumefanya nini kumfanya Rais wetu kuwa kinara? Inabidi tukae tuzungumze kwa pamoja nini kinatukwamisha? Kwa nini tupeleke pamba nje badala ya nguo? Rais Samia ameamua, ni lazima tuamue kwenda kutoa huduma kimataifa,” alisema Dkt. Kijaji.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bw. Ally Gugu amesema Tanzania ni sehemu rasmi ya Mkataba wa AfCFTA ambapo nchi wanachama pamoja na sekretarieti wameanzisha nyenzo inayotengeneza mazingira rahisi kwa walioibaini fursa kuwawezesha kuuza. Hivyo aliyetayali kufanya biashara atume taarifa zake katika batua pepe ya afcfta.gti@mit.go.tz

Nao Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI), Bw. Leodger Tenga,
Mkurugenzi Mkuu – TPSF Bw. Gilead Teri na Nebart Mwapwele
Kaimu Mkurugenzi Mkuu – TCCIA pamoja wamesema wapo tayari kuchangamkia fursa ya soko hilo linalokadiriwa kuwa na watu bilioni 1.4 lenye pato la pamoja ya thamani ya dola trilioni 1.2

Wakurugenzi hao wametakiwa wafanyabiashara watanzania kuja na mpango wa bidhaa kumi muhimu kwa ajili ya kuuza katika eneo huru la biashara Afrika ifikapo julai mosi 2023.

Aidha, Baadhi ya Wafanyabiashara Watanzania walioshiriki mkutano huo walijitokeza na kusema wako tayali kuanza kupeleka bidhaa zao ikiwemo Kahawa na Katani katika Soko la AfCFTA .