Site icon A24TV News

JUMUIYA YA WAZAZI TAIFA YAMPONGEZA RAIS SAMIA TAMKO LA MIKUTANO YA HADHARA

Na Geofrey Stephen Arusha

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Fadhili Maganya amempongeza Rais Dk,Samia Hassan Suluhu kwa kutoa ruhusa ya kuanza kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa nchini

Aidha amesititiza kuwa ziara za nje wanazofanya Rais Dk, Samia zinaleta tija zaidi kwani akirudi nchini harudi bure na zinafungua milango nje na ndani ya nchi.

Maganya aliyasema hayo leo Jijini Arusha wakati Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutoa tamko la umoja huo.

Alisema fursa ya mikutano ya hadhara iliyotolewa na Rais Samia ni kuonyesha namna bora ya kuendesha siasa hapa nchini.

Alisema Rais amesema mikutano ya vyama vya siasa itumike kukosoa bila kugombana ikiwemo kuanza kukwamua mchakato wa katiba.

Alisema pia Rais ameridhia kuendelea kuangalia sheria mbalimbali kwaajili ya kuziboresha kwa maslahi mapana ya nchi na kuahidi ushirikishwaji wa wadau na makundi mbalimbali katika kuziboresha sheria hizo

“Tunatoa wito kwa watanzania wote kumtia moyo Rais Samia kwani umoja na mshikamano ndio msingi wa maendeleo katika nchi yetu”

Alitoa rai kwa vyama vya siasa kuzingatia sheria,kanuni na miongozo mbalimbali katika utekelezaji wa shughuli za siasa hapa nchini ikiwemo kumuunga mkono kwakuendeleza siasa za maridhiano kwa maslahi mapana kwa mustakabali wa nchi.

Akizungumzia kuhusu safari anazozifanya Rais Samia nje ya nchi,Maganya alitumia methali ambazo ni mgaa,gaa na upwa hali wali mkavu na kusema kuwa mwenda bure si mkaa bure ,hivyo Rais anaposafiri kunafursa mbalimbali anafungua.

Kuhusu mikopo wanayodai anakopa kopa sana,Maganya alisisitiza kuwa Rais anakopa kwa maslahi ya Taifa na nchi kwa ujumla na mikopo inafanya kazi na kazi zinaonekana.

Mwisho