Site icon A24TV News

CCM NA SERIKALI SAMBAMBA KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI IKUNGI

Na Mwandishi wa A24Tv.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ikungi Nd. Mika Tano Likapakapa ameongoza wajumbe wa kamati ya siasa, Sekretariati pamoja na mkuu wa wilaya ya ikungi Mhe. Jerry C. Muro na mwenyekiti wa halmashauri ya ikungi Mhe. Ali Mwanga na watendaji kutoka halmashauri ya ikungi wameanza ziara ya siku tano ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika kata ya kintuntu

Katika ziara hiyo ambayo pia ilijumuisha vikao vya ndani vya kiutendaji baina ya wajumbe wa halmashauri za vijiji na uongozi wa ccm kuanzia tawi na kata wananchi walipata nafasi ya kupewa taarifa ya utendaji kazi na miradi inayotekelezwa katika wilaya na haswa kata ya kintuntu na kisha kupewa nafasi ya kutoa kero na malalamiko waliyonayo.

Akizungumza katika kata kintuntu Ndungu Mika amesema wamelazimika kuwafuata wananchi walipo akiwa na kikosi kazi kamili kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa ilani ya chama ikiwemo kusikiliza na kutatua kero zao papo kwa papo hatua ambayo itakisaidia chama kujua utendaji wa serikali katika ngazi za kata na vijiji.

Baadhi ya wananchi wamepongeza hatua ya mwenyekiti wa ccm wilaya kuanza ziara na kikosi kazi kamili ambacho kimejumuisha viongozi wote waandamizi wa serikali na chama hatua ambayo inawasaidia wananchi kutatuliwa kero zao kwa haraka

Kwa upande wao mkuu wa wilaya ya ikungi Mhe. Jerry C. Muro na mwenyekiti wa halmashauri Mhe. Ali Juma Mwanga mbali na kujibu na kufafanua mambo mbalimbali ambayo yameonekana kuwa kero kwa wananchi wamesema kazi yao ni kuhakikisha wanayafikia maeneo yote ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya mwenyekiti wa ccm taifa ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wananchi wanafikiwa na kutatuliwa kero zao kwa haraka

Katibu mwenezi wa ccm wilaya ya Ikungi Ndugu Nassoro Henku amesema ratiba za mikutano hiyo zitatolewa na kutangazwa na viongozi wa ccm wa kata na matawi pamoja na wenyeviti wa vijiji na kwa siku ya kesho Jumanne tarehe 17/01/2023 kikosi kazi kitakuwa kata siuyu kijiji cha makotea na kata ya lighwa

Mwisho