Site icon A24TV News

13 MBARONI KWA UCHAKACHUAJI MBOLEA NJOMBE WAKIWEMO WANAWAKE WAWILI

Na Mwandishi wa A24Tv Njombe

Jeshi la polisi mkoani Njombe linawashikilia watu 13 akiwemo mhusika mkuu wa uchakachuaji mbolea za ruzuku na kuwauzia wakulima baada ya msako mkali wa takribani wiki mbili.

Mbele ya vyombo vya habari Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa Amesema awali walikamatwa baadhi ya wafanyakazi wa wakala huyo ambaye jina lake limehifadhiwa lakini sasa na yeye amekamatwa tayari.

Aidha Kamanda Issa Amesema kati ya watu hao 13 waliokamatwa wawili ni wanawake pamoja na waliokuwa wakisafirisha vifaa vya kufanikisha uchakachuaji huo wa mbolea na wauzaji wa maduka.

Wakati hayo yakijiri katika Jeshi la polisi mkoani Njombe baadhi ya madiwani wilayani Wanging’ombe akiwemo Geofrey Nyagawa katika kikao maalum cha baraza la madiwani cha kupitisha rasimu ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 wamesema kilichofanyika na mkuu wa mkoa wa Njombe kuendesha msako huo chini ya vyombo vya ulinzi na usalama kinapaswa kufanyika kwa nchi nzima kwani madhara yake